Mkurugenzi Manispaa Morogoro ataka Jamii kutambua mchango wa Watoto.
MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, ameziomba Jamii kutambua mchango wa watoto kuelekea siku ya Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika.
Hayo ameyazungumza leo Juni 15, 2020 Ofisini kwake ikiwa imebakia siku moja kuelekea katika kuaadhimish aSiku ya Mtoto wa Afrika .
Akizungumza na Waandishi wa habari, Lukuba, amesema moja ya kuwajali Watoto ni pamoja na kufanya uhamasishaji kupinga ukatili kwa watoto hususani mila ya ukeketaji ambayo inaathiri kwa namna mbalimbali maslahi ya watoto katika jamii.
Katika maadhimisho ya mwaka huu 2020 dhima kuu kwa Afrika ni "Mifumo Rahisi ya Upatikanaji wa Haki ya Mtoto:Ni Msingi Imara wa Kulinda Haki zao".
'"Kesho tunaadhimisha maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, yapo mengi ya kuyafanya katika kuwalinda Watoto wetu, lakini tukumbuke changamoto kama vile migogoro ya kifamilia, masuala ya UKIMWI, malezi ya watoto, ukatili wa kijinsia, ndoa, mirathi naajira hivi vyote vina wanyima haki watoto , niwaombe Wananchi wa Mnaispaa ya Morogoro, kipindi hiki Watoto wetu wapo nyumbani likizo, niombe kuna kazi za kuwatumikisha lakini hawa tukiwategemea katika kazi za uzalishaji wa mali hatuwatendei haki, lazima familia katika kipindi hiki tuangalie kwa umakini matendo tunayoyafanya nyumbani, natumaini siku hii itakuwa chachu ya Mkombozi kwa Watoto wetu" Amesema Lukuba.
Lukuba, ameendelea kuwataka wananchi wa Manispaa ya Morogoro na Watanzania kuheshimu na kulinda haki za watoto kwa kuzingatia kwamba haki za watoto zimekuwa hatarini.
Hata hivyo ameziomba Jamii na Familia kuwashirikisha watoto katika kufanya maamuzi yanayogusa maslahi yao ili kufanya maamuzi sahihi kwa kundi hilo.
Aidha, ameukumbusha umma wa watanzania kuachana na mila kandamizi zinazodidimiza maslahi ya mtoto na badala yake kulinda haki za watoto hasa kwa kuzingatia watoto ni moja ya makundi yanahitaji ulinzi mbadala.
Ikumbukwe kwamba kila ifikapo Juni 16 kila mwaka bara la Afrika huadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika tangu kuidhinishwa kwa siku hiyo na Umoja wa Afrika mwaka 1991 ambapo Umoja wa Afrika ulianzisha Siku ya Mtoto wa Afrika kama sehemu ya kuwakumbuka na kutambua mchango wa watoto waliopoteza maisha katika mauaji yaliyotokea huko Soweto, Afrika ya Kusini wakati watoto walipoandamana kudai haki zao za msingi.
Ikumbukwe kwamba kila ifikapo Juni 16 kila mwaka bara la Afrika huadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika tangu kuidhinishwa kwa siku hiyo na Umoja wa Afrika mwaka 1991 ambapo Umoja wa Afrika ulianzisha Siku ya Mtoto wa Afrika kama sehemu ya kuwakumbuka na kutambua mchango wa watoto waliopoteza maisha katika mauaji yaliyotokea huko Soweto, Afrika ya Kusini wakati watoto walipoandamana kudai haki zao za msingi.
Post a Comment