AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA MOROGORO MJINI ATANGAZA SIKU 4 ZA ZOEZI LA WAZI DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA. .
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI UWEKAJI WAZI DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA.
AFISA Mwandikishaji Jimbo la Morogoro Mjini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogro , Sheilla Lukuba, ametangaza Siku 4 za zoezi la wazi la Daftari la Wapiga kura kwa Waanchi wa Jimbo la Morogoro Mjini ambapo zoezi hilo linatarajiwa kuanza tarehe 17 hadi 20 /06/2020.
Tangazo hilo limetolewa leo Juni 15, 2020 , Ofisini kwake na kusema kuwa vituo vitakavyotumika ni vile vituo vilivyotumika wakati wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga Kura.
Lukuba, amesema kuwa Uwekaji wazi huo utafanyika kwa kuzingatia tahadhari zote za afya kuhusu kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na Virusi vya Corona.
Aidha, amesema wahusika katika zoezi hilo ni pamoja na Wapiga Kura wote walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mwaka 2015, walioandikishwa wakati wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Kwanza na ya Pili kwa Mwaka 2019/2020, Wapiga Kura hawa ni wale ambao hawakuhakiki taarifa zao wakati wa uwekaji wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura awamu ya kwanza.
Amesema kuwa, Wapiga kura watakao hakiki taarifa zao kwenye Daftari la Awali la Wapiga Kura lilipowekwa wazi na kukuta picha zao hazipo wanatakiwa kwenda kwenye KITUO CHA SHULE YA MSINGI MWERE KATA YA KINGO kilichoandaliwa na Afisa Mwandikishaji Jimbo la Morogoro Mjini ili wapigwe picha nyingine na kupewa kadi.
Hata hivyo, amesema kuwa iwapo mpiga Kura amehakiki taarifa zake kwa kutumia njia yoyote kati ya hizo nne na kutaka kufanya marekebisho ya taarifa zake atatakiwa kwenda katika Kituo kilichopangwa na Ofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na kufanya marekebisho hayo.
Amesema kuwa Kituo kitakachohusika na marekebisho kilichopo cha Shule ya Msingi Mwere) itahusisha watu kama vile , Mpiga Kura anayehitaji kumuwekea pingamizi Mpiga Kura asiye na sifa za kuwemo katika Daftari la Awali la Wapiga Kura ataenda katika Kituo kilichopangwa. , Wapiga kura wanatakiwa kutoa taarifa za ndugu waliofariki dunia ili waondolewe kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Aidha amesema mambo yafutayo hayatahusika Katika zoezi hilo , miongoni mwa vitu hivyo ni pamoja na Uandikishaji wa Wapiga Kura Wapya, hakutakuwa na Uboreshaji wa Taarifa za Wapiga Kura waliohama maeneo yao ya kiuchaguzi, waliopoteza kadi au kadi zao kuharibika.
UTARATIBU WA UHAKIKI Mpiga kura anaweza kuhakiki taarifa zake kwa njia zifuatazo:- 1. Mpiga Kura mwenyewe kufika katika kituo alichojiandikisha na kuhakiki taarifa zake katika orodha itakayokuwa imebandikwa katika kituo hicho. Mtu mmoja kwenye familia anaweza kukagua taarifa za familia nzima. 2. Mpiga Kura kupitia simu yake ya kiganjani kupiga namba *152*00# na kufuata maelekezo yatakayo mwezesha kuhakiki taarifa zake. 3. Mpiga kura kupiga simu namba 0800112100 na kufuata maelekezo yatakayo mwezesha kuhakiki taarifa zake. 4. Mpiga Kura kuhakiki taarifa zake kupitia Tovuti ya Tume, www.nec.go.tz kwa kubonyeza sehemu iliyoandikwa ‘uhakiki’ na kuendelea kufuata maelekezo. MAMBO YA KUZINGATIA 1.
Taarifa hii imetolewa na: Sheilla E. Lukuba Afisa Mwandishaji Jimbo ya Morogoro Mjini.
Post a Comment