DC Chonjo atatua mgomo wa Wafanyabiashara Soko la Mawenzi Manispaa ya Morogoro.
MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, ameutatua
mgomo wa Wafanyabiashara wa Soko la Mawenzi Manispaa ya Morogoro baada ya
kuingilia kati na kuwaomba Viongozi kukaa meza moja kwa ajili ya kutatua mgogoro huo.
Tukio hilo la mgomo la Wafanyabiashara hao limefanyika leo
Juni 04, 2020 kwewnye Soko hilo huku baadhi ya Wafanyabiashara wakijawa na
taharuki na sintofahamu kufuatia wenzao kuitwa Kituo cha Polisi baada ya kupokea barua ya wito kutoka kwa Kamanda wa Polisi Wilaya ya Morogoro juu ya
Mgogoro huo.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Chonjo, amesema kuna
taarifa za upotoshaji zilifanyika juu ya wito wa wafanyabiashara 12
walionadikiwa barua ya kuhitajika Kituo cha Polisi Wilayani .
Chonjo ,amesema wito huo ulikuwa na nia njema sana kwa
wafanyabiashara hao lengo ni kujua ni changamoto gani wanakabiliana nazo katika
Soko lao na kujua ni kwa namna gani wanaweza kufanya suluhu ya Mgogoro huo.
"Hivi
kweli ukamataji wa Polisi ni kutumiana barua? Lengo la Polisi ni
kuwaita ili kujua kuna kitua gani kinaendelea na kujadili kwa pamoja, hivyo
niwatoe hofu kuitwa kwao Polisi ilikuwa njia njema na pengine wangekwenda
ilikuwa ni kueleza kero na changamoto zinazolikabiri Soko la Mawenzi “ Amesema
DC Chonjo.
Mbali na barua za wito kwa Wafanyabiashara hao, zilizuka hoja mbali mbali zinazohusiana na Wafanyabiashara hao ambazo zote zilihitaji ufafanuzi wa kina kutoka kwa Mkuu wa Wilaya.
Akijibu
hoja ya mafanyabiashara aliyetaka kujua juu ya hatima ya eneo la la TTCL
ambalo waliliomba kipindi cha Utawala wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ,
Mhe. Stephen Kebwe, DC Chonjo, amesema ni kweli kuwa TTCL waliandika barua la
kulitaka eneo lao.
“Ni
kweli TTCL wameandika barua ya kulitaka eneo lao, na sisi Uongozi tumewaomba
kwa kutambua waliopo hapo ni watu na wanatafuta ridhiki , na ombi letu
walituambia tujenge vibanda ambavyo sio vya kudumu, sasa sisi tumewaomba watupe
muda na kuona jinsi ya kuwapanga wafanyabiashara wetu namna ya kupata ridhiki na
hili ombi la muda na bahati mbaya hawakutujibu tunaendelea kuwaomba lakini tunaimani baada ya wiki mbili zijazo Soko letu Kuu la
Kimkakati litakuwa tayari , na wale wa Manzese tutawarudisha Sokoni na watakao
taka kuomba Manispaa itatoa tangazo kwa ajili ya maombi hayo” Amesema DC
Chonjo.
Kuhusu
hoja ya Malori makubwa kutofika Mjini
kushusha mizigo, amesema kwa sheria za TARURA na TANROADS, na kanuni
walizoziweka Manispaa ya Morogoro Malori makubwa hayatakiwi kuingia kwenye
barabara ndogo.
“Agizo
linasema magari yenye uwezo wa tani 3 kushuka chini ndiyo yatakayoruhusiwa
kuingia ndani ya miji na kwenye Masoko yote ya Manispaa , lakini nasikitika
sana Wataalamu wetu hawajatutendea haki , kama agizo ni tani 3 kuja Mawenzi,
kibali cha tani 3 kutoka nanenane cha nini? Kuchukua kibali cha tani 3 ni
ukiritimba na unachelewesha watu kutofikisha bidhaa zao kwa wakati na kusababisha hasara ” Ameongeza
DC Chonjo.
Mwisho,
amepiga marufuku ushushwaji wa mizigo usiku , huku akisema jambo hilo sio
sahihi , lakini akalumu kutokuwepo kwa wawakilishi katika vikao vya kimaamuzi
ambapo jambo hilo linasababisha kutotolewa kwa taarifa sahihi kwa
wafanyabiashara ambao wanategemea mapokeo kutoka kwa Uongozi wao.
Kwa
upande wa Kamanda wa Polisi Wilaya ya Morogoro, (OCD) Jackson Kahamba, amesema
wajibu wake ni kulinda watu pamoja na mali zao hivyo anavyopata taarifa juu ya
sintofahamu anawajibu wa kufuatilia na kujua yaliyopo ili kuweza kuchukua
maamuzi kwa mujibu wa sheria na kanuni za Jeshi la Polisi.
“
Nilipata taarifa ya sintofahamu juu ya makundi mawili ambayo baadae yataleta
tafrani, kwa dhamana niliyokuwa nayo nikaona niwaandikie barua hawa wawakilishi
wan wanaoshusha mizigo ili tuweze kujua
nini chanzo na tupate suluhisho ili maisha yaendelee kama kawaida,ila siku na
lengo la kuwakamata , ningekuwa na lengo hilo pasingekuwa na haja ya
kuwaandikia barua ningetuma askari
kawakamateni kama majina
yalivyokuwa yameainishwa, niwaondoe hofu na sijawahi kuweka mtu nandi kwa
sababu haya ni mambo yanayotakiwa
kuyajadili na kuyapatia ufumbuzi” Amesema OCD Kahamba.
Kwahiyo kwa Sasa Hali shwari na Wafanyabiashara wanaendelea Kama kawaida kutoa huduma.
Kwahiyo kwa Sasa Hali shwari na Wafanyabiashara wanaendelea Kama kawaida kutoa huduma.
Post a Comment