Header Ads

Kamati ya Fedha Manispaa Morogoro ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga  (aliyevaa suti nyeusi) akiwa pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Fedha mara baada ya kuwasili katika eneo la ujenzi wa Stendi ya Daladala Kaloleni.

Mhandisi wa TARURA Manispaa ya Morogoro na msimamizi wa miradi inayofadhiliwa na Benki Kuu ya Dunia, James Mnene akitoa maelezo ya miradi  kwa wajumbe wa Kamati ya Fedha.
Wajumbe wa kamati ya Fedha wakipatiwa maelezo ya miradi na Msimamizi wa miradi inayofadhiliwa  na   Benki Kuu ya Dunnia James Mnene.

Wajumbe wa kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro  leo tarehe 09/06/2020 wamefanikiwa kutembelea miradi 3 inayoendelea kutekelezwa.
Miradi hiyo ni Ujenzi wa Soko Kuu la Kisasa, Stendi kuu ya Daladala Mafiga, Jengo la Kitegea Uchumi pamoja na Stendi ya Daladala Kaloleni.
Kamati hiyo iliongozwa na Mhe. Pascal Kihanga ,  Mstahiki Meaya wa  Halmashauri ya Morogoro na Diwani wa Kata ya Mazimbu.
Mhe. Kihanga, amewashukuru wasimamizi wa miradi katika sekta mbalimbali kwa kuonyesha moyo wa uzalendo katika utekelezaji wa miradi hiyo na kuwataka watendaji wa Halmashauri kuipitia Mara kwa Mara miradi inayotekelezwa ili iweze kuleta tija kwa Wananchi.


















No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.