KAMATI ya Siasa CCM Wilaya Morogoro yaridhishwa na utekelezaji wa miradi ya Maendeleo Manispaa ya Morogoro.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Morogoro Mjini wakikagua eneo la kuchinjia Kuku katika Soko Kuu la Kisasa.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Morogoro Mjini wakikagua ujenzi wa Soko Kuu la Kisasa Manispaa ya Morogoro.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga (kulia) akiteta jambo na Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro , Sofia Kibaba (katikati) wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Morogoro Mjini wakipatiwa maelezo juu ya Ujenzi wa Soko Kuu la Kisasa.
Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro , Sofia Kibaba (kushoto) akiwa pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Siasa CCM Wialaya ya Morogoro Mjini, Chausiku Lukinga (kulia) wakikagua Choo cha walemavu katika ujenzi wa Soko Kuu la Kisasa.
Ujenzi wa Paa la Jengo la Kitega Uchumi DDC Manispaa ya Morogoro ukiendelea.
Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Juma Gwisu akiwaonesha wajumbe wa Kamati ya Siasa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini maeneo ya Ujenzi wa Stendi ya Daladala Mafiga.
Muonekano wa Vyoo vya Soko Kuu la Kisasa .
KAMATI ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Morogoro , imeridhishwa na hali utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa katika halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa CCM Wilayani Morogoro, Ndg. Fikiri Juma, alipokuwa katika ziara ya siku moja ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyofanyika tarehe 03/06/2020 katika maeneo ya Stendi ya Kisasa ya Daladala Mafiga, ujenzi wa Soko Kuu la Kisasa uliopo Kata ya Mji Mkuu pamoja na Jengo la Kitega Uchumi DDC Kata ya Kingo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari , amesema kasi na ubora wa Ujenzi unaonesha dhahiri Manispaa imekimbizana na inastahili pongezi ya hali ya juu kwani licha ya ubora lakini imeonesha ni jinsi gani imezingatia thamani ya pesa iliyotumika.
Akizungumza na Waandishi wa Habari , amesema kasi na ubora wa Ujenzi unaonesha dhahiri Manispaa imekimbizana na inastahili pongezi ya hali ya juu kwani licha ya ubora lakini imeonesha ni jinsi gani imezingatia thamani ya pesa iliyotumika.
Fikiri , ambae pia ndiyo mwenyekiti wa kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Morogoro, amesema wamefanya ziara hiyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Irani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi na kwamba miradi yote waliyoitembelea ipo katika hatua nzuri ya utekelezaji, jambo linaloleta matumaini makubwa katika matumizi sahihi ya fedha za miradi hiyo ambayo kimsingi inatekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Aidha, amesema kuwa , miradi yote waliyotembelea ikiwamo wa Soko Kuu la Kisasa , Stendi mpya ya Daladala Mafiga pamoja na Jengo la Kitega Uchumi DDC yote imetekelezwa kwa kufuata viwango vya hali ya juu.
Fikiri, amemuomba Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro pamoja na Mkurugenzi kuhakikisha wanaweka Uongozi imara katika miradi hiyo ili iweze kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia usawa , haki na kufuata misingi ya sheria.
Amesema kuwa miradi yote waliyoikagua katika ziara ya kawaida imeonesha thamani ya pesa iliyotumika , huku akiuomba Uongozi wa Manispaa ya Morogoro kuweka mikakati mathubuti ya ukusanyaji wa fedha katika miradi hiyo.
""Serikali imetupatia miradi mikubwa ya Kimkakati, miradi hii ni kwa ajili ya kuongeza mapato ya Manispaa , sasa niseme tu tuitumie miradi hii kwa manufaa makubwa sana, isije kuwa Serikali imetuletea neema ikageuka matatizo dhidi ya Wananchi inatakiwa tujipange kuanzia ngazi za usimamizi na ukusanyaji mapato lakini kubwa ni kufanya kazi pamoja na kuleta maendeleo chanya yaliyokusudiwa na Serikali kwa kutoa hudma kwa Wananchi " Amesema Fikiri.
Hata hivyo, Mwenyekiti Fikiri amempongeza Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Juma Gwisu pamoja na Mhandisi wa TARURA Manispaa ya Morogoro, James Mnene kwa kazi nzuri wanazozifanya katika kusimamia ubora wa miradi.
Aidha Fikiri, ameitaka Halmashauri kuendelea kuwa wabunifu, na kuisimamia kikamilifu stendi hiyo ili kuongeza Mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kuwa nia na matokeo ya mradi huo ni kuongeza Mapato kwa Halmashauri pamoja na kutoa huduma kwa wananchi.
Mwisho, ameshuri Uongozi wa Manispaa ya Morogoro, kuongezwe ruti za vituo kwa ajili ya wasafiri ili baadaye isijekuleta manung'uniko na Wananchi.
"Kumekuwa na changamoto sana ya ruti za daladala ndani ya Manispaa yetu jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa sana, Mstahiki Meya na Mkurugenzi kaeni muone hili mnaliweka katika njia gani iliyobora ili haya manungúniko yasiwepo, nishauri kabla ya kukamilik akwa Soko, angalieni uwezekano wa kuweka stendi ndogo ya daladala iliyojirani na Soko kwa ajili ya kushushia abiria ili iwe rahisi kwao kuifuata huduma" Ameongeza Fikiri.
Kwa upande wa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, ameishukuru Kamati ya Siasa ya Wilaya kwa kutekeleza majukumu yao kusimamia vyema Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM.
Kihanga amesema ,amewataka Wananchi wa Manispaa ya Morogoro kuitunza na kuilinda Miradi hiyo mara itakapokamilika ili iweze kudumu na kuwanufaisha na kuweza kupata maendeleo ya Kiuchumi na kijamiii na kuondoa umasikini kwa Watanzania.
""Nimuombe Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro pamoja na Menejimenti yake wafanye kazi kwa pamoja ili kuweza kusimamia miradi hiyo huku akisema kwamba jukumu la Watendaji wote Serikalini ni kufanya kazi kwa weledi na kuwajibika kwa kila nyanja ili kuweza kuwaletea Wananchi maendeleo kupitia miradi mbalimbali ikwemo Sekta ya Afya ,Usafiri , Elimu na Sekta zingine za miundombinu ya barabara na maji'' Amesema Kihanga.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa stendi hiyo, Msimamizi wa Miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia, Mhandisi James Mnene, kwa niaba ya Mkurugenzi amesema kuwa, Mradi huo Umetekelezwa kwa gharama za Tshs Bilioni 4.4 bila VAT ambapo mpaka sasa Mkandarasi ameshalipwa Shilingi Bilioni 3.6 sawa na asilimia 82 ya bajeti ambayo amaelipwa.
“Tunapenda kuishukuru sana Serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli, kwa kuipatia fedha Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya ujenzi wa Kituo hiki,mpaka sasa Mkandarasi ameshalipwa Shilingi Bilioni 3.6 sawa na asilimia 82 ya bajeti amabyo wamelipwa kati ya Bilioni 4.4 ambazo ni gharama ya mradi bila VAT , matarajio yetu wiki mbili zijazo tuwe tumeukabidhi mradi huu Manispaa na wananchi waanze kuutumia mradi huu” Amesema Mnene.
Mnene, amesema mpaka sasa Ujenzi wa Stendi hiyo umefikia asilimia 98,ambapo kazi zilizobakia ni kazi za usafi pamoja na matengenezo ya vitu vidogovidogo kama vile utenegenezaji wa Bustani kwa ajili ya kuweka manzari yaonekane vizuri.
Mnene, amesema mpaka sasa Ujenzi wa Stendi hiyo umefikia asilimia 98,ambapo kazi zilizobakia ni kazi za usafi pamoja na matengenezo ya vitu vidogovidogo kama vile utenegenezaji wa Bustani kwa ajili ya kuweka manzari yaonekane vizuri.
"Utekelezaji wa mradi hii mpaka sasa tunaenda vizuri licha ya kuwepo kwa changamoto za hapa na pale, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hatua tulizofikia , ni matumanini yangi ndanii ya kipindi cha mwezi huu mmoja uliopo, miradi yote tunakwenda kuikamilisha ili Wananchi waendelee kunufaika na miradi yao kwa kupata huduma" Amesema Mhe. Kihanga.
Post a Comment