DC Chonjo atoa wiki 2 kuvunjwa kwa vibanda vya Mabanzi nje ya Stendi Msamvu.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, akikagua Vibanda vilivyoungua na Moto kufuatia hitilafu ya umeme nje kidogo ya Kituo cha Mabasi Msavu. |
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo,(kushoto), Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba (kulia), Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro , Mhe. Pascal Kihanga (kushoto mwa DC Chonjo) na viongozi wengine wakifuatilia kwa makini eneo la vibanda vilivyoungua moto.
Vibanda vilivyoungua kufuatia hitilafu ya umeme Kituo cha Mabasi Msavu. |
Guzo la Umeme ambapo imetokea hitilafu ya umeme lilopo nje ya Kituo cha Mabasi Msavu eneo la geti la kuingilia Mabasi. |
MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, ametoa muda
wa siku 14 kwa wafanyabiashara waliojenga Vibanda vya mabanzi nje kidogo ya Stendi
ya Mabasi Msavu wayavunje ili waingie ndani ambapo ndipo maeneno yametengwa kwa
ajili yao .
Kauli hiyo ameitoa mei 31, 2020 wakati wa ziara ya kukagua
vibanda ambavyo viliungua na moto kufuatia
kutokea wa hitilafu ya Umeme.
Akizungumza na Waandishi wa habari, amesema Serikali
imetengeneza miundombinu inayokubaliaka inayoendana na Stendi hiyo ya
kisasa kwa kuweka fremu nzuri ambazo
zinapangishwa kwa wafanyabishara.
Chonjo ,amesema vibanda hivyo vilivyojengwa kiholela vinaweza kusababisha hasara kubwa ya uwekezaji wa kitega uchumi chenye thamanai ya shilingi Bilioni 24 jambo ambalo amelikemea vikali na kuwataka wafanyabiashara hao kuhamia ndani kwa kufuata utaratibu uliopangwa na Uongozi wa Stendi ya Mabasi Msamvu.
Amesema kuwa licha ya kutambua kuwa wafanyabiashara hao wanatafuta ridhiki lakini amewaambia ridhiki nzuri ni ile inayotafutwa mahali kwenye usalama na sio eneo ambalo wao wametengeneza vibanda vyao ambavyo vinahatarisha maisha ya Stendi nzima inapotokea janga la moto.
“Nawapa wiki mbili
yani siku 14, Mabanda haya ya Mabanzi yaliyopo eneo hili tusiyakute , yaondosheni nendeni kwenye
maeneno ambayo yametengwa na hii Stendi, haikujengwa kwa miundombinu
ya namna hii,Meneja wa Msamvu wachukue hawa wapangisheni, hata wakikaa watatu
fremu moja sio mbaya mbona hapa nasikia wanakaa hadi watatu na wanalipa kodi, hizi
sehemu mlizoweka mabanda zinasomeka kama sehemu za miti na maua kwa ajili ya
kupumzika wananchi wa Manispaa ya
Morogoro,lakini hata huu umeme ni wa uwizi haiwezekani Meneja wa TANESCO awapitishie umeme kienyeji namna hii kwa kupitisha chini kwenda kwenye Mabanda “ Amesema DC Chonjo.
Chonjo, amesema watakapoingia ndani itawarahisishia kujua biashara zao zinakwendaje, na kujua ni kwa muda gani mabasi yana simama kwa ajili ya kupata huduma.
“”Nakumbuka ajali ya moto iliyotokea mwaka jana,bahati mbaya
hakuna aliyejua kama itatokea ajali wengi mlikimbilia huko mkasema mnafuata
utajiri , lakini kilichotokea ni vilio, sasa kama hapa nako kukitokea hivyo ni
hatari hatuwezi kuhatarisha maisha ya wananchi wetu kwa jambo ambalo halikubaliki , hivyohivyo nyinyi mkiuungua na eneo hili likiteketea atakayewajibishwa
ni mimi inapotokea janga hili , nimetoa siku 14 kama bado mimi nikija na
vibomoa vyote, tukubali kufuata utaratibu uliowekwa” Ameongeza DC Chonjo.
Aidha, amesema kama Moto huo ungeunguza vibanda vyote na
stendi hiyo imezungukwa na vituo vya mafuta na kuna mabasi ya abiria ambayo
yanapita na vyombo hivyo vina mafuta , basi wangekuwa wanazungumzia janga
jengine la moto la Msamvu.
Hata hivyo, amemuagiza Meneja wa TANESCO kukatisha mawasilinao
ya umeme katika Vibanda vyote vya
wafanyabiashara Stendi ya Msamvu kwani njia walizotumia katika kuunganisha
umeme sio salama.
Aidha, amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, ndani
ya wiki mbili kazi ya kuweka miundombinu ya kurejesha ramani ya Stendi ya
Msamvu kama ilivyokuwa iwe imeanza kwa ajili ya usalama wa Stendi, wananchi
pamoja na Jengo lenyewe.
Naye Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Morogoro, ACP Goodluck Zelote, amesema kuwa mabanda yaliyoungua sana ni mawili ambayo yalikuwa yamehifadhia vitu vya wafanyabiashara wengine , lakini kikubwa walichokifanya ni kuzima moto na hatua iliyopo kwa sasa ni kuweza kujua gharama ya vitu ambavyo vimeteketea kwa Moto ili tuone kuna hatua gani itachukuliwa” Amesema ACP. Zelote.
Post a Comment