VISHOKA NA MADALALI WATAHADHARISHWA MRADI WA SOKO KUU LA KISASA MANISPAA YA MOROGORO.
Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Michael Waluse (kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro , Mhe. Abood na watumishi wengine katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Manispaa ya Morogoro.
MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa , amewataka wafanyabiashara wasiokuwa na biashara (VISHOKA) katika mradi wa Soko Kuu la kisasa linalotarajiwa kufunguliwa kutojihusisha na
upangaji wa fremu wala Vizimba .
DC Msulwa ametoa agizo hilo leo Juni 25, 2020 wakati wa ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo Manispaa ya Morogoro ikiwemo Ujenzi wa Soko Kuu la Kisasa , Stendi Mpya ya Daladala Mafiga pamoja na Stendi ya Kaloleni.
“Kama huna biashara , huwezi kupangisha katika maeneo yetu ya Soko, tafsri ya haraka haraka wewe ni kishoka au dalali , maana utakuwa una wanyonga wale wenye uhitaji wakati wewe unatumiwa na watu, hatutaki vishoka katika miradi yetu, hii ni miradi ya wananchi, tunatambua ujanja wenu wa nyani, niwaagize Manispaa wekeni utaratibu wenu utakao wafanya wananchi wakapata maeneno haya kwa njia nzuri yenye amani, hatutokuwa tayari kumuingiza mtu ambaye anatumia mgongo wa mwenzake kuwanyonya wengine, simamieni hili ili mradi huu uweze kuwanaufaisha wananchi kama ilivyokusudiwa, jukumu lenu ni kufuatilia, kukemea na kuchukua hatua stahiki penye udhaifu na si vinginevyo,” Amesema DC Msulwa.
Amesema kama wapo watu wananmna hiyo hatawafumbia macho atahakikisha hawapati nafasi ya namna hiyo kwani kufanya hivyo ni kinyume na matarajio ya Soko hilo na kuwanyima haki wenye haki za kunufaika na mradi huo ambao ni kodi za Wananchi wanyonge.
Amesema ni vema kila mdau au kiongozi akatimiza wajibu wake ipasavyo katika kusimamia sheria na kanuni na utaratibu ili yale malengo ya kunufaisha wananchi yasije kugeuka vyanzo vya migogoro katika Wilaya yetu na Mkoa kwa ujumla.
Hata hivyo, amesema ameridhishwa na kasi ya miradi ya Manispaa ya Morogoro inayoendelea ambapo amewaomba Wakandarasi wa miradi hiyo kukimbizana na muda ili kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.
Amewaagiza wadau wote wanaohusika na mradi wa Soko kukutana nao kesho saa 1:30 kwa ajili ya kuangalia wapi wanakwama na ni njia gani zitumike ili mradi huo ukabidhiwe kwa wananchi.
Amesema kipindi hiki lazima wakhakikishe wataalamu wataalamu kwa kushirikiana na wakandarasi wanaongeza kasi zaidi kukamilisha miradi yote kwa wakati ili wananchi waendelee kupata huduma .
Mwisho ametoa wito kwa Wataalmu wampatie taarifa ya thamani ya miradi yote, ubora wa miradi, muda wa kukamilika kwa miradi pamoja.
Kazi nzuri sana
ReplyDelete