MANISPAA YA MOROGORO YAUNGA MKONO JUHUDI ZA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI
MANISPAA ya Morogoro imesema itaendelea kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO), ili kuharakisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Morogoro, Ennedy Mwanakatwe, akimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa katia uzinduzi wa Mtandao wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (MUNGONET) uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kilakala Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro.
Mwanakatwe, amesema serikali inatambua mchango wa mashirika hayo nchini katika kuleta maendeleo huku akiyahakikishia kutoa ushirikiano.
“Serikali inatambua mchango wa NGO, hivyo niwahakikishie serikali ipo tayari kuendelea kushirikiana nanyi,” Amesema Mwanakatwe.
Naye Mwenyekiti wa MUNGONET, Mwajabu Dhahabu, amesema kikao hicho kimetoa njia na mwongozo katika kuboresha utendaji kazi na majukumu wa mashirika hayo.
Mwajabu amesema Serikal ikitumia TEHAMA itapunguza gharama na mfumo wa kutumia makaratasi kuandaa ripoti, mfumo ambao hupoteza muda.
Pia katika uzinduzi huo, wadao hao walijadili juu ya kuondoa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.
Post a Comment