MEYA KIHANGA ATOA KWA WATU WENYE UALBINO WALIOPATIWA MITAJI.
MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amewataka wanufaika 19 waliopatiwa mitaji kwa watu wenye Ualbino Manispaa ya Morogoro kuhakikisha wanatumia mitaji hiyo kwa kutekeleza malengo waliyojiwekea.
Kauli hiyo,ameitoa,
Septemba 6/2022 wakati wa hafla fupi ya utoaji wa ruzuku kwa watu wenye Ualbino
kupitia ufadhili wa ADRA Tanzania katika Ukumbi wa DDC Mbaraka Mwinshehe
Manispaa ya Morogoro.
‘’
Ninawaomba sana mitaji hii mliyopewa mkaitumie kwa malengo mliyojiwekea,kuna baadhi ya watu wanatabia wanapopewa mitaji au mikopo hii hubadiri mawazo na malengo yao na kuamua kuzigawana fedha kwa matumizi
binafsi,kumbukeni wafadhili wetu wametoa matarajio yao ni kuona fedha hizi
zinazaa matunda, lakini niwaombe mkajiunge vikundi Manispaa inatoa asilimia 10
ya makusanyo ya mapato ya ndani ya kila mwezi ili kuwawezesha wananchi kujikwamua
kiuchumi, na njia nzuri ya ilionekana kupitia vikundi , Imani yangu mtafanya
vizuri kwa kuwa tayari nimesikia mshapata mafuzo juu ya biashara zenu” Amesema
Mhe. Kihanga.
Kwa upande
wa Mkurugenzi wa ADRA Tanzania, Sam Oyortey, amesema
bado kuna kundi kubwa la watu wenye ulemavu wanaopaswa kuwezeshwa ujuzi na
mitaji ili waweze kujitafutia kipato.
Oyortey, ameiomba Manispaa ya Morogoro licha ya
walemavu hao kupatiwa mitaji lakini Manispaa ijikite katika kuona namna ya
kuwaongezea mitaji katika mikopo yao ya asilimia 2.
Naye Mwenyekiti wa Watu wenye Ualbino Mkoa wa Morogoro, Hassan
Mikazi, amesema kukosekana kwa mitaji kwa watu wenye ulemavu umesababisha wengi wao wanakosa fursa mbalimbali ambazo
zingeweza kupunguza viwango vya umasikini.
Post a Comment