Header Ads

BMK KATA YA MAFIGA YAKABIDHI KADI ZA BIMA YA AFYA KAYA 100 KWA WAZEE.






BARAZA la Maendeleo Kata ya Mafiga, limewezesha kaya 100 za wazee  kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) iliyoboreshwa  ambapo malengo yao ni kuona wazee wanaendelea kupata huduma za afya bure kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Kadi hizo zimetolewa katika maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika Kata ya Mafiga eneo la Kituo cha Afya Mafiga.

Akizungumza mara baada ya mgeni rasmi kukabidhi kadi hizo, Diwani wa Kata ya Mafiga, Mhe. Thomas Butabile, amesema kuwa wameamua kufanya hivyo kwa lengo la kutimiza ahadi ikiwa ni pamoja na kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi CCM.

“Tumetoa  Bima hizi kwa kaya 100 mpaka sasa lakini kaka yangu Mhe. Chomoka  amenihakikishia kadi 100 nyengine hii ni hatua kubwa ya kuona sasa tunakwenda kuhakikisha wazee wetu wanapata  huduma ya Afya kwa uhakika mwaka mzima” Amesema Butabile.

Mwisho, Mhe. Butabile amewataka wananchi wa Kata ya Mafiga  kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii.

Kwa upande wa Wazee ambao  ni wanufaika wameshukuru jitihada za diwani na Baraza lake la Maendelep   kwa kuwawezesha kujiunga na mifuko ya Bima ya Afya huku wakisii viongozi wengine kuiga mfano huo.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.