Header Ads

RC MWASSA AAHIDI KUENDELEZA MICHEZO MOROGORO

MKUU wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwassa amesema Ofisi yake ipo tayari kuendeleza michezo mbalimbali katika Mkoa huo kwa sababu ya ukweli kuwa michezo ni afya lakini pia michezi ni ajira.

Fatma Mwassa amesema hayo Agosti 22 mwaka huu 2022  wakati akikabidhiwa makombe ya ushindi kwa vijana walioshiriki michezo ya UMITASHUMTA na UMISETA na kufanya vizuri hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

Akifafanua zaidi Mkuu huyo wa Mkoa amehaidi kuendeleza vipaji kwa vijana hususani kwenye mcheo mbalimbali ikiwemo ya mpira wa miguu handball na Goalball pamoja na michezo mingine akiamini kuwa kupitia michezo hiyo vijana wanaweza kujiajiri.

Kwa upande wake Mkuu wa WIlaya ya Kilosa Majid Mwanga amewapongeza vijana walioshiriki mashindanao hayo hususani wenye mahitaji maalumu kwa kufanya vizuri zaidi kushika nafasi ya kwanza ya mchezo wa Goalball huku akiwahakikishia kuwapa msaada wa hali na mali kwenye mashindano yajayo ya AFcon.

Akitoa taarifa ya mashindano hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa Katibu Tawala Msaidizi ambaye pia ni Afisa Elimu wa Mkoa wa Morogoro Bi. Germana Mung’aho amesema timu ya Mkoa wa Morogoro kwa upande wa UMISSETA imefanikiwa kupata makombe 5 na kuwa mshindi wa 5 Kitaifa na kwa upande wa UMITASHUMTA Mkoa umefanikiwa kupata jumla ya makombe 4 na medali 3 na kuwa mshindi wa 5 Kitaifa. Hivyo Mkoa wa Morogoro kwa ujumla umefanikiwa kupata makombe 9 na medali 3 kwa mashindano hayo ya UMISETA NA UMITASHUMTA


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.