MANISPAA YA MOROGORO KUENDELEA KUBORESHA HUDUMA BORA KWA WAZEE.
MANISPAA ya Morogoro itaendelea kujiimarisha katika kuboresha upatikanaji wa huduma bora kwa wazee kwa kuzingatia umuhimu wa kundi hili katika jamii.
Hayo yamesemwa na mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Hamisi Ismail ambaye ni Kaimu Afisa Tarafa Manispaa ya Morogoro katika maadhimisho ya siku ya wazee duniani Manispaa ya Morogoro yaliyofanyika Septemba 24/2022 katika Ukumbi wa maonesho wa SUA Nanenane.
Aidha, ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kuboresha maisha ya wazee ili kuhakikisha wanapata huduma jumuishi na stahiki kwa ajili ya ustawi na maendeleo yao, ikiwemo kuboresha utoaji wa huduma kwa wazee kuwa ni moja ya vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
" Serikali inatambua kuwa wazee ni hazina katika kuibua na kuchochea shughuli mbalimbali za kimaendeleo kutokana na ushauri mzuri wanaotoa wanaposhirikishwa katika mambo ya kimaendeleo,"Amesema Hamisi.
Kwa upande wa Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Morogoro, Sidina Mathias, amesema Manispaa ya Morogoro itaendelea kujiimarisha katika kuboresha upatikanaji wa huduma bora kwa Wazee kwa kuzingatia umuhimu wa kundi hili katika jamii yetu.
" Manispaa yetu ya Morogoro kwa kuwatambua Wazee wameanza kutatua changamoto ya vitambulisho vya msamaha wa matibabu bure kwa wazee wetu hii ni hatua muhimu sana katika Ustawi wa Wazee" Amesema Sidina.
Naye Mratibu wa Wazee Manispaa ya Morogoro, Rehema Malimi, ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wazee hao juu ya UVIKO-19 na kuwataka wazee kuendelea kuchanja, kwani wapo kwenye kundi ambalo ni rahisi kupata maambukizi hayo huku akiwatoa hofu kwamba chanjo hii ni salama kabisa na kuwataka kumuunga mkono Mhe.Rais alieona umuhimu wa kuokoa maisha ya watanzania kwa kupata chanjo hii.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo , Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Manispaa ya Morogoro , Rashid Zongo, amepongeza maadhimisho hayo huku akizitaja kiwilaya ndani ya kata ya Bugogwa, Mzee Jackson Kabote ambaye ni katibu wa baraza la wazee wilaya ya Ilemela amezitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili wazee ikiwa ni pamoja upungufu wa dawa na wa wataalam wa kuhudumia wazee,umaskini uliokithiri kutokana na kipato duni au kutokuwa na kipato kabisa sambamba na wazee kutokupewa kipaumbele kama makundi mengine kama vile wanawake,vijana na walemavu.
Post a Comment