Header Ads

SOMA NA MTI YAZIDI KUPAA MANISPAA YA MOROGORO, MITI ZAIDI YA 100 YAPANDWA SHULE YA MSINGI MBUYUNI.


KAMPENI ya Soma na Mti imeendelea leo Aprili 04/2022 katika Shule ya Msingi Mbuyuni Manispaa ya Morogoro ambapo katika kampeni hiyo zaidi ya Miti 100 imepandwa.

Kampeni hiyo ya Soma na Mti imekuwa mara ya pili kuzinduliwa  kwani kwa mara  ya kwanza ilizinduliwa katika Shule ya Sekondari Mbuyuni kwa upande wa shule za Sekondari.

Kampeni hiyo kwa upande wa Manispaa ya Morogoro imekuwa ikiratibiwa na Moro Mazingira kwanza kwa kushirikiana na Balozi wa Mazingira Tanzania, Bw Chage kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Mazingira  Manispaa ya Morogoro ikiwamo TFSA na wadau wengine.

Soma na Mti kwa sasa imelenga zaidi katika upandaji wa miti katika shule mbalimbali zikiwamo za Msingi na Sekondari.

Malengo ya Soma na Mti ni kuhakikisha kila shule inaotesha miche kwa kuwa na vitalu vya kuotesha miche  ili kufanikisha kampeni hiyo na kufikia shule nyingi zaidi.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.