Header Ads

WATU WENYE ULEMAVU WAPEWE NAFASI.



KATIKA  jumla ya watu wote dunia nzima inasemekana kuwa asilimia 10 ni walemavu. Ulemavu unaweza kutokana na mtu  kuzaliwa nao, ajali , magonjwa yanaopeleka kiungo cha mwili kukatwa au kushindwa kufanya kazi. 

Kila kiungo cha binadamu kinaumuhimu wake sana katika maisha yetu ya kila siku mfano miguu kutembelea macho kuona masikio kusikia na n.k.

Mtu anaposhindwa kutumia viungo vyake katika maisha ya kila siku ndi tunaita ulemavu. Ulemavu mara nyingi utokea wa kudumu na Mara chache sana kunawanaobahatika kupona mfano wenye ulemavu wa kusikia kutokana na kuumwa saaingine wanaweza kubahatika kupona na n.k


Kwa kuwa kila kiungo cha mwili wa binadamu kina umuhimu wake katika maisha yetu ya kila siku mtu anapokuwa na ulemavu wa viungo anapata changamoto kufanya shughuli inayotakiwa kufanyika na hicho kiungo cha mwili.

Mbali na changamoto ya ulemavu walemavu wanazopitia lakini wanakutana na changamoto kubwa ya ubaguzi.Zifuatazo ni aina mbalimbali za ubaguzi walemavu wanazokutana Nazo

UBAGUZI KATIKA SHUGHULI ZA KIJAMII walemavu wanakutana na ubaguzi sana katika shughuli za kijamii.Mara nyingi huchukuliwa kama watu wasiojiweza na wasioweza kuleta mabadiliko katika jamii jambo ambalo sio kweli.walemavu wanaweza na wanaouweza wa kushiriki shughuli mbalimbali na kuleta matokeo chanya katika jamii

UBAGUZI KATIKA SHUGHULI ZA KIUTAMADUNI Kuna jamii zenye utamaduni mbaya ambao wenye athari sana kwa walemavu. Kuna jamii wanaaoamini kuwa na ulemavu ni laana wengine wanaamini ni mkosi kwa hiyo wanawatenga na kuwatesa watu wenye ulemavu. Kuna jamii ambao uwafungia ndani walemavu kwa kuogopa kuwa wanawatia aibu . Na cha kuhuzunisha kuna jamii ambao uwauwa watoto wanaozaliwa na ulemavu wakiamini wanaepuka laana jambo ambalo sio kweli.

UBAGUZI KATIKA KUSHIRIKI SHUGHULI ZA KIUCHUMI. Watu wenye ulemavu pia wanahaki ya kushiriki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi.Sema jamii zetu zimejiaminisha kuwa watu wenye ulemavu ni watu wasiojiweza watu tegemezi, kitu ambacho sio kweli watu wenye ulemavu wanaweza kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi na kujiingizia vipato kwa njia halali na pia wanahaki ya kumiliki mali wanazozitafuta.

Kuna kitu cha kusikitisha kuna watu wanawatumia watu wenye ulemavu kama vitega uchumi vyao. Wanawalazimisha watu wenye ulemavu kwenda kuombaomba kwa watu alafu wanachukua hizo hela wanazozipata huu ni ukatili ambao kila mtu anatakiwa aupinge vikali.Watu wenye ulemavu sio kwamba hawajiwezi kabisa kunabaadhi ya vitu wanaweza kufanya vizuri na kujiingizia kipato halali. Mfano pale soko kuu Arusha kuna mkaka ambaye ni kipofu.Lakini pia ni mmachinga anauza viberiti vibanio vya kubania nguo na n.k. Yeye ni mfano hai kuwa walemavu wanaweza.
Akishikwa mkono na kupewa nafasi anaweza kufanya kufanya vizuri zaidi kwa kuwa anaweza na ajaruhusu ulemavu kuwa kikwazo kwake.

UBAGUZI KWENYE KUPATA AJIRA. Ni nadra sana kuona mtu mwenye ulemavu ameajiriwa. Makampuni mengi mashirika hayawapi nafasi watu wenye ulemavu nafasi katika kampuni zao wakiamini hawana uwezo ni kitu ambacho sio kweli. Unakuta mtu ana cv nzuri inayomuwezesha kupata kazi lakini akishasema kuwa yeye ni mlemavu basi anakosa ajira. 

Hiki ni kitu cha kuhuzunisha kwani watu wenye ulemavu pia wanahaki ya kuishi maisha yao kuwa na familia kuishi kama mtu wa kawaida.  kampuni yake inayoitwa fuwavita ambao wanatengeneza siagi za karanga , mvinyo na n.k.

Watu wenye ulemavu wanahitaji elimu ambayoitawasaidia katika maisha yao ya baadae. Elimu ni muhimu katika maisha yetu. Watu wenye ulemavu wanahitaji elimu bora ili waelimike na kuweza kutatua matatizo yanaowakabili.

Ni jambo jema kwamba dunia sasa inatambua umuhimu wa elimu kwa watu wenye ulemavu na kuwasaidia mbinu mbalimbali za kujifunzia mfano lugha ya vitendo kwa wasiosikia na pia wasioona wanavitabu vyao maalumu vya kusoma .

Kwa kuwa elimu ni muhimu sana kwa jamii serikali na wadau wanapaswa kusaidiana ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata elimu bora picha ya nne inaonyesha matokeo ya kidato cha nne mwaka 2017 ambayo yaliwauzunisha wadau wengi. Lakini ni hatua gani zilichukuliwa baada ya aya matokeo ? Je waliobaki walisaidiwaje wasipate matokeo yasiorizisha tena.? Je awo wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia waliopata matokeo yasio mazuri walisaidiwaje ili kujiandaa maisha yao ya baadae mfano kupewa elimu ya ujuzi au kwenda vyuo vya masomo ya vitendo...?.

 Pia inawezekana kabisa kwa wanafunzi wenye ulemavu kupata alama nzuri na elimu bora endapo wakiangaliwa kwa ukaribu mfano aliekuwa mkuu wa wilaya ya kisawire alianzia kampeni ya tokomeza zIro kisawire na kampeni yake ilifanikiwa vizuri. 

Kwa hiyo wanafunzi hata wenye ulemavu wakiangaliwa kwa ukaribu wanaweza kufanya vizuri katika elimu yao.

Elimu na ujuzi kwa watu wenye ulemavu ni muhimu sana inawasaidia kutokuwa tegemezi na inapunguza ubaguzi. Mfano chuo cha ujasiriamali cha Arizona kinachopatikana mikocheni dar katika harambee ya choo salama ya madam Sophia ilitoa scholarship maalumu kwa watu wenye ulemavu ili wapatiwe elimu ya ujasiriamali ili waweze kuendesha maisha yao ya kila siku kwa kufanya ujasiriamali.

Lakini pia kuna taasisi mbalimbali zinaowasaidia walemavu kama ya Dr Leginald Mengi foundation aliyoanzisha hayati Dr Mengi ili kuwasaidia walemavu katika shughuli zao za kiuchumi na kijamii na n.k.

Pia kwa kujua haki za walemavu katiba yetu ya Tanzania mwaka 1977 ilianzisha sheria inayowalinda watu wenye ulemavu zidi ya ubaguzi.

Kuna mfano mingi kuwa watu wenye ulemavu wanaweza lakini hawapewi nafasi au jamii yao haiwasapoti na changamoto nyingi wanazokumbana Nazo za kuwafanya wajione hawawezi na wao ni tofauti.

Inaweza ikawa watu wenye ulemavu hawawezi kufanya kila kitu lakini kuna baadhi ya vitu wanaweza kufanya vizuri sana na kikamilifu.

Jamii inapaswa kupewa elimu ya kuwa watu wenye ulemavu wanaweza na wakipewa nafasi wanaweza kufanya vizuri nakuwa ulemavu sio mkosi wala laana.pia watu wenye ulemavu ni sawa na watu wengine wasitengwe wala kubaguliwa.

Watu wenye ulemavu wanahaki ya kuajiriwa , kutoa maono, kushiriki shughuli mbalimbali za kitaifa pia kushiriki siasa na hata kuwa viongozi.

Watu wenye ulemavu wanatakiwa wapewe nafasi kwani wanaweza kufanya kazi nzuri zenye kuleta matokeo chanja katika jamii.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.