AJIRA JUMUISHI- WALEMAVU WASIWE WA ZIADA.
WATU wenye ulemavu Tanzania ni kundi dogo la watu wasiozidi hata 2,000,000 kwa bara na visiwani ila ni kundi linaloongoza kutaabika mitaani ukiachana na Makundi ya Wagonjwa,Wafungwa na Wakimbizi hapa Tanzania.
Kumekuwa na changamoto kubwa sana katika jamii na taasisi zetu juu ya watu wenye ulemavu kutoweza kushiriki kwa pamoja katika ajira jumuishi hii imetokana na mitazo tofauti toafauti juu yao.
Lakini, suala la walemavu kutokuingia katika ajira jumuishi limekuwa kikwazo kwao kwani wengi wao wamekuwa wakiishi katika maisha tegemezi jambo ambalo limekuwa likiwaathiri kisaikolojia na kuathiri mazingira yao na hata kufikia wakati kutojiona kwamba wao sio sehemu ya jamii kutokana na kutengwa kwao.
Hali ya wanawake na wanaume walemavu kwenye soko la ajira linatia hofu na mashaka makubwa kwani wana fursa ndogo zaidi ya kuajiriwa kuliko wasio walemavu na hata wakiajiriwa wengi wao huwekwa katika sekta ambazo malipo yake ni haba.
Sekta ya Ajira.
Tanzania kupitia jitihada za Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Awamu ya Nne, iliweka sheria maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu ijulikanayo kama "Sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010".
Katika sheria hiyo baadhi ya mambo mazuri yaliainishwa yahusianayo na masuala ya Ajira kwa Watu wenye ulemavu hususani kwenye Ibara ya 31 na 32.
Swali :
-Ni Taasisi ngapi za Serikali zenye jumla ya wafanyakazi 300ambao kati ya hao 9 ni watu wenye ulemavu???
-Je Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kama chombo pekee kinachoratibu michakato ya Ajira serikalini kinawajibikaje kwa Waajiri wa taasisi za Umma ili kuhakikisha sheria hii inatekelezwa kikamilifu??
-Je ni kweli kwamba Sekretarieti ya Ajira katika utumishi wa umma hausiki kwa namna yoyote ile na utekelezaji wa sheria hii kama anavodai Naibu Katibu wake???
2.Kila mwajiri ahakikishe anapeleka ripoti ya utekelezaji wa sheria ya watu wenye ulemavu kuhusu waajiriwa wake ambao ni watu wenye ulemavu kwa Kamishna wa Kazi kila mwaka.
Swali :
-Ni waajiri wangapi wa taasisi Binafsi na Umma wanawasilisha ripoti hizo kwa Kamishna kila mwaka??
-Kama jibu ni ndiyo je huwa wanawasilisha ripoti sahihi kwa kkiasi gani??
-Je ripoti hizo huwa zinafanyiwa kkazi ??
-Kama jibu ni ndiyo kwann idadi kubwa ya watu wenye ulemavu wasio na Ajira inazidi kuongezeka kila kukicha??
-Je waajiri huwa huwa wanakaguliwa kuhusiana na utekelezaji wa sheria hii ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010,Sheria ya kazi ya mwaka 2004 na Mkataba wa kimataifa wa Watu wenye ulemavu wa mwaka 2010??
Bado naendelea kutoa na kuwahamasisha walemavu kuchangamkia fursa za ajira zinazotangazwa na Ofisi ili waweze kupata fursa .
Mfumo wa elimu maalumu unaweza kuchangia baadhi ya watoto kukosa haki za msingi kutokana na umri lakini pia kupoteza asili na tamaduni zao kwa kusoma mbali na nyumbani kutokana na wazazi wengi kuwapeleka watoto shule maalumu na kuwatelekeza watoto huko.
Hivyo ushauri wangu ni kwamba tuendelee kutoa elimu juu ya kuwepo kwa mfumo wa elimu jumuishi kwa watoto wenye mahitaji maalumu kuchanganyikana na wengine ujambo ambalo litasaidia sana kutengeneza umoja na kuondoa unyanyapaa kwa kuwa tayari wamezoeana na kupendana pamoja na kupewa ushirikiano kutoka kwa wenzao.
Post a Comment