Header Ads

EGG TANZANIA YAWAKUMBUKA ALBINO, YAGAWA VIFAA NA MAVAZI KWA AJILI YA KUJIKINGA NA MIONZI YA JUA .

 ASASI ya kiraia ya Education Gauge for Growth Tanzania (EGG )yenye Makazi yake Kata ya Mazimbu manispaa ya Morogoro  wamegawa vifaa na mavazi kwa watu wenye Ualbino ikiwa na lengo la kuwasaidia katika kujilinda na mionzi ya jua.

Zoezi hilo la ugawaji limefanyika April 22/2022 katika uzinduzi wa Ofisi mpya ya Chama Cha watu wenye Ualbino Mkoa wa Morogoro TAS.

Akizungumza mara baada ya kugawa vifaa hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa EGG Tanzania, Jumanne Mpinga, amesema wameamua kufanya hivyo ikiwa na lengo la kuweza kuwalinda katika miili yao dhidi ya mionzi ya jua.

Kapinga amesema Egg Tanzania imekuwa na desturi ya kugawa Vifaa hivyo mara kwa mara kwa watu wenye ualbino ikiwa ni sehemu ya kuwatia faraja na moyo katika kuona wao wana haki sawa na watu wengine.

" Huu ni uratibu wetu kama Ofisi, tumeanza kugawa vifaa hivi Wilaya ya Kilosa na leo tupo Manispaa ya Morogoro baada ya kupata mwaliko huu na ndugu zetu wa TAS tukaona tuwaunge mkono kwa hiki ambacho tumejaliwa nacho kwa hawa ndugu zetu" Amesema Kapinga.

Miongoni mwa vifaa ambavyo Egg Tanzania wamevitoa ni Losheni za jua pisi 200, Kofia za kuzuia mionzo ya jua 50, Miwani 50 , nguo 50 za kike na za kiume pamoja na Miamvuli 50.

Mbali na misaada hiyo, Egg Tanzania inafanya kazi mikoa yote na pia imekuwa ikijihusisha na utoaji pia wa misaada mbalimbali ikiwamo uchimbaji wa Visima vya maji haswa Shuleni. 

Naye Fadhila Juma mwenye Ualbino,ameishukuru Egg Tanzania kwa msaada huo huku akisema bado wanakabiliwa na changamoto hivyo amewaomba wadau wengine wajitokeze kuwasaidia.



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.