Header Ads

TAS -MOROGORO YAZINDUA OFISI MPYA, DIWANI KANGA AAHIDI KUSIMAMIA HAKI ZA ALBINO KATIKA KUWEKA USAWA WA HAKI

Diwani wa Kata ya Kilakala, Mhe. Marco Kanga, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ofisi Mpya ya Chama Cha Albino Mkoa wa Morogoro (TAS-MOROGORO), (kushoto) Afisa Ustawi Manispaa ya Morogoro, Rehema Malimi, ( Mwenyekiti wa SHIVYAWATA TAIFA na Mwenyekiti Mstaafu wa TAS Taifa na Diwani wa Kata ya Chumbageni Tanga), Mhe. Ernest Kimaya.

Diwani wa Kata ya Kilakala, Mhe. Marco Kanga,(aliyekaa) akiwa katika  Ofisi ya Mweka hazina wa TAS-Mkoa wa Morogoro.

Diwani wa Kata ya Kilakala, Mhe. Marco Kanga,akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa TAS-Mkoa wa Morogoro.

Diwani wa Kata ya Kilakala, Mhe. Marco Kanga,(wapili kutoka kulia), Mkurugenzi Mtendaji Asasi ya kiraia ya Egg Tanzania, Jumanne Mpinga (kushoto) wakimkabidhi mwamvuli wa kjizuia na jua Mwenyekiti wa TAS Mkoa wa Morogoro, Hassan Mikazi (katikati), (kulia) Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro , Jesca Kagunila.

Mkurugenzi Mtendaji Asasi ya kiraia ya Egg Tanzania, Jumanne Mpinga , akizungumza wakati wa kuendesha zoezi la ugawaji wa vifaa kwa watu wenye Ualbino.


CHA Cha Watu wenye Ualbno Mkoa wa Morogoro (TAS), kimezindua Ofisi Mpya iliyoko Mtaa wa Nugutu , Kata ya Kilakala Manispaa ya Morogoro.

Uzinduzi huo umefanyika April 22/2022 ambapo mgeni rasmi alikuwa Diwani wa Kata ya Kilakala, Mhe. Marco Kanga,  kwa niaba ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga.

Aizungumza mara baada ya uzinduzi wa Ofisi hiyo, amesema kitendo cha TAS- Morogoro kuwa na Ofisi yao kitarahisisha upatikanaji wa huduma bora hususani kwa wale wanufaika ambao TAS imekuwa ikiwahudumia.

Aidha, Mhe. Kanga , ameupongeza Uongozi wa  TAS -Morogoro kwa hatua waliyofikia na kusema kuwa  Serikali ipo pamoja na kutambua  jitihada zote zinazofanywa na Viongozi wa TAS kuanzia ngazi ya Taifa hadi Wilaya na  kwamba Serikali itaendelea kutambua umuhimu wa  viongozi pamoja na kulinda haki za Albino kwa kutengeneza misingi imara ya kuweka uwiano mzuri wa haki.

Licha ya hapo, amesema bado kumekuwa na viashiria vibaya juu ya watu wenye Ualbino ya jamii kutokuwa na uelewa na kuanza kuwanyanyapaa jambo ambalo linakosesha watu hao kutopata huduma zao za msingi na kufanyiwa vitendo vya unyanyapaaji.

" Leo hii, Karne ya Sayansi na Teknolojia, Watanzania tunawabagua Walemavu wa Ngozi, tunawakata viungo na kuwaua Ndugu zetu kwa imani za Kishirikina. Hii ni dhambi ambayo hatutasamehewa kwa Mungu. Naomba Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu  Mkoa wa Morogoro kaka yangu Mikazi Hassan usimame. Hivi huyu Bwana mbali na yeye kuwa Mweupe na mimi Mweusi tuna tofauti gani nyingine? Mungu amemuumba kama mimi. Kampa viungo vyote kama mimi. Sasa imani za Kijinga kuwa ukipata Kiungo cha Albino utakuwa tajiri zinatoka wapi? Kama ingekuwa hivyo, kwa nini msiende Nchi za Ulaya na Asia kwa sababu Mabara hayo yana Watu wengi wenye Ngozi Nyeupe ili muwe Matajiri. Nami leo nawaambia Watanzania wote hususani Wananchi wa Manispaa ya Morogoro  kwamba Mungu ametuumba sote kwa Mfano wake tuachane na imani Potofu za Kishirikina. Ameongeza Mhe. Kanga.

Aidha, Kanga, ameipongeza Serikali kwa kuchukua hatua za kupiga vita dhidi ya mapamabano ya vitendo vya ukatili kwa Watu wenye Ulemavu wa ngozi (Albinism).

Kanga, amesema moja ya hatua zilizochukuliwa na Serikali ni pamoja na kuitisha Kura ya Maoni kwa nia ya kuongeza kasi na nguvu ya Mapambano dhidi ya Vitendo vya Ukatili kwa Watu wenye Ulemavu wa Ngozi ambapo Serikali iliwataka Wananchi kutaja Watu wanaowajua kuwa wanajihusisha na Mauaji au kukata Viungo vya Watu wenye Ulemavu wa Ngozi, wawataje Waganga wa Jadi wanaohusika, Wauaji, Wauzaji wa Viungo na Wafanyabiashara wanaotumia Viungo hivyo.

Hata hivyo ,Mhe. Kanga, aliupongeza Uongozi wa Egg Tanzania kwa kujitolea Mafuta ya ngozi kwa Albino, mavazi pamoja na fedha za nauli kwa walengwa wenye Ualbino  ambapo amesema wanastahili kuigwa na wamekuwa wadau wakubwa wanaojitoa katika shughuli mbalimbali za Maendeleo  za Kuiunga mkono Serikali pamoja na watu binafsi au mmoja mmoja.

Pia, amechukua  nafasi hiyo kuanza  kuzishukuru Taasisi zote za Serikali na zisizo za Kiserikali zikiwemo Taasisi za Dini ambazo zimeshiriki kuwasaidia Watu wenye Ulemavu Nchini hususani Manispaa ya Morogoro kwa  kuona umuhimu wa kusadia kundi hilo muhimu katika Jamii. 

Mwisho, ametoa wito kwa Taasisi mbalimbali kwa kuwakumbusha na kusisitiza kwamba Watu wenye Ulemavu wanahitaji msaada mkubwa kutoka kweo, hivyo wanahitaji misaada na ushirikiano  wa kuwapatia mahitaji yao muhimu ikiwa ni pamoja na Elimu, Huduma za Afya na Mazingira mazuri ya kuwawezesha kuishi bila ya matatizo huku akisema  Serikali kwa upande wake itajitahidi kwa uwezo wake kutoa fursa zinazojali mahitaji yao. 

Naye , Mwenyekiti wa TAS-Mkoa wa Dar Es Salaam, Hassan Mikazi,ameuopongeza Uongozi wa TAS-Tiafa kwani wamekuwa wakishirikiana vyema katika kulete chachu ya Maendeleo.

Mikazi, amesema licha ya ufunguzi wa Ofisi bado wanakabiliwa na changamoto kama vile vitendea kazi, vifaa vya Ofisini na Samani ya vifaa ikiwamo Meza, Viti, Laptop, n.k.

" Tulianza na chumba kimoja , lakini tunashukuru Mungu wadau wetu wa Voice Global wameweza kutupambania na kuhakikisha tunapata huduma kubwa ya kuwa na Ofisi yetu ni jambo kubwa wametufanyia na wanaendelea kutufanyia, tunaomba Serikali na  wadau wengine wajitokeze ili tuzidi kuendelea kuwahudumia ndugu zetu wenye Ualbino" Amesema Mikazi.




No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.