KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.
WAJUMBE wa Kamati ya Huduma za Uchumi ,Afya na Elimu Manispaa ya Morogoro , wamefanya ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo huku wakionesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo.
Ziara hiyo imefanyika tarehe 11/4/2022 na kutembelea Ujenzi wa Zahanati Mpya ya Mgaza iliyopo Kata ya Mindu na ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Kata ya Mindu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofautii , wajumbe hao wamepongeza jitihada za serikali katika kihakikisha huduma zinawafikia wananchi wake kwani hatua ya miradi yote ipo hatua nzuri.
sambamba na hayo Wajumbe hao wameagiza Uongozi wa Manispaa kuhakikisha kwamba Zahanati zote zilizokamilika zianze huduma za awali ili miradi hiyo iendele kuwahudumia wananchi wakati huduma nyengine zikisubiriwa kukamilika.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kingo, Mhe. Amini Tunda, amewashukuru wajumbe kwa ziara hiyo huku akiwahahakikishia kusimama kidete kuoana miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Mhe. Tunda, amempongeza Diwani wa Kata ya Mindu, Mhe. Zuberi Mkalaboko, pamoja na Uongozi wake wa Kata kwa kusimamia vyema miradi hiyo.
Kwa upande wao, miongoni mwa wajumbe hao, Mhe. Latifa Ganzeli, amesema ni vyema sasa baadhi ya Zahanati ambazo zimeshakamilika zianze kutoa huduma ili wananchi waweze kufaidi matunda ya kodi zao.
Naye, Diwani wa Kata ya Mindu, Mhe. Zuberi Mkalaboko, amesema miradi yote inaendelea vizuri na Uongozi wa Kata ya Mindu umekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanasimamia vyema miradi hiyo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Ally Machela,amesema miradi hiyo ipo katika hatua nzuri , na upande wa Zahanati mpya nyengine zimeshaanza kutoa huduma ikiwamo Zahanati ya Tungi.
Post a Comment