MBUNGE MZERU AWATAKA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI KUHUBIRI ZAIDI AMANI YA TANZANIA.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Mzeru, akimkabidhi Baba Paroko Parokia ya Dakawa , Father. Drazan Klapez, (katikati) fedha taslimu laki 3 kwa ajili ya kuchangia Flashi ya albamu ya nyimbo za Injili.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Mzeru, akiwa katika picha ya pamoja na Baba Paroko Parokia ya Dakawa , Father. Drazan Klapez, katika sanamu ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere , sanamu ambayo imechongwa na Kanisa hilo.
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Mzeru, amewataka waimbaji wa nyimbo za injili nchini kuhubiri zaidi amani ya Tanzania katika tungo zao.
Mhe. Mzeru, ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa wa Albamu ya Nyimbo za Dini Kwaya ya Mtakatifu Joseph Dakawa Wilaya ya Mvomero April 24/2022.
Aidha, Mh. Mzeru, amesema kuwa amani ni jambo la muhimu sana, Mataifa mengi yamekuwa katika machafuko kwa sababu ya kukosa Amani, hivyo kama Wanakwaya wanawajibu sasa katika tungo zao wakaanza kuwa na nyimbo za kuhamasisha amani ili kila Mtanzania atambue thamani ya kuilinda amani katika maeneo yao.
Hata hivyo,Mhe. Mzeru, amewaomba viongozi wa dini wasichoke kuwalea Vijana katika maadili, kwani wamekuwa wakitengeneza Taifa imara lenye upendo ndani yake, huku akisema Serikali inatambua wa kazi zao wanazozifanya katika jamii na kuahidi kwamba Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi zao na kuwa pamoja nao katika majukumu yao ya kuwalea Vijana katika amani.
" Ndg. Baba Paroko Parokia ya Dakawa ,kwanza nipende kutoa shukrani zangu za Dhati za kunialika katika hafla hii ya uzinduzi wa Albamu ya Nyimbo za Dini Kwaya ya Mtakatifu Joseph, niseme hii ni nafasi ya upendeleo kwangu na imenipa faraja sana kuona hata viongozi wetu wa Dini wamekuwa wakitambua sana umuhimu wetu kwa jamii kwa kazi ambazo tumekuwa tukizifanya, napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba Waimbaji wa injili , kuhubiri zaidi amani ya nchi yetu, Amani ni muhimu sana jamani, mkitumia kipaji chenu hiki kuhubiri Amani , Taifa letu litaendelea kuwa na Umoja , upendo na Mshikamano" Amesema Mhe. Mzeru.
" Leo tupo katika uzinduzi huu wa Albamu wa nyimbo za Injili Kwaya ya Mtakatifu Joseph, ni vyema sasa Waimbaji wetu wakaanza kutumia vyema fursa waliyonayo kwa kuimba nyimbo zenye kuhamasisha Amani na upendo nchini katika tungo zao, nimeona kwenye barua yenu albamu yenu yenu ni nzuri sana ya ‘NI NANI MWENYE UPENDO WA KWELI’? sasa kwa vile mmeipa jina hilo mnatakiwa sasa muonesho upendo wenu wa kweli kwa kuhubiri Amani lakini pia msiache kuliombe Taifa letu, Viongozi wetu wa Vyama na Serikali pamoja na Rais wetu mpendwa Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kutimiza majukumu yake kwani amekuwa akijitoa kuhakikisha Taifa hili linabakia katika taswira nzuri ya ramani kwa kuwa na Amani Duniani kote" Ameongeza Mhe. Mzeru.
Katika hatua nyengine, Mhe. Mzeru, amechukua nafasi hiyo kutanguliza salamu za Mkoa wa Morogoro na kusema Serikali itaendelea kushirikiana na Viongozi wa Dini kuhakikisha wanalinda amani iliyopo na kuwalea Vijana katika Maadili sahihi na yaliyo mema katika kujenga Taiafa jema kwa maendeleo yetu.
Mwisho , amewaomba sana Viongozi wa dini, kuendelea kuhimiza waumini na umma , juu ya zoezi la Sensa linalotarajia kuanza hivi karibuni na kusema ni vyema sasa kupitia viongozi hao wa dini wakawa katika mstari wa mbele kuhimiza jamii kujitokeza kuhesabiwa mara zoezi hilo litakapoanza kwani Sensa ndio mpango wa maendeleo yetu na vizazi vyetu lakini pia viongozi hao kutoa ushirikiano mkubwa kwa zoezi linaloendelea kwa sasa la Anwani za Makazi ambalo Rais , Mhe. Samia Suluhu Hassan ,amelipa heshima kubwa kwa ustawi wa maendeleo yetu.
Naye Baba Paroko , Parokia ya Dakawa , Father Drazan Klapez, amemshukuru Mhe. Mzeru kwa kuwa pamoja nao katika uzinduzi wa albamu yao.
Fz, Klapez, amesema kupitia ushirikiano wa viongozi wa Serikali ni dhahiri wataweza kuhakikisha wanawajenga Vijana kiroho ili kuweza kumjua Mungu.
Katika uzinduzi huo, Mhe. Mzeru alitoa kiasi cha pesa shilingi laki 3 taslimu kwa ajili ya kuwaunga mkono waimbaji wa injili katika mauzo yao ya albamu huku akiahidi kutatua changamoto nyengine .
Post a Comment