Header Ads

RC SHIGELA APIGA MARUFUKU WAFANYABISHARA KUPANDISHA BEI ZA VYAKULA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI.









MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Martine Shigela, amepiga marufuku wafanyabishara kupandisha bei za vyakula wakati huu wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

RC Shigela, amepiga marufuku Aprili 13/2022 baada ya kufanya ziara ya ghafla katika soko kuu la Chifu Kingalu  Manispaa ya Morogoro  ili kuona bei za vyakula.

 “Sio mpandishe bei ya vyakula kwa sababu tu ni mwezi Mtukufu wa Ramadhani, uzeni kwa bei halali bei ambayo mlikuwa mnauza tangu awali,” Amesema Shigela.

Amewataka Wakala wa Vipimo Manispaa ya Morogoro  kupita kwenye Masoko yao  ili kuona namna wateja wanavyopimiwa vyakula.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.