Header Ads

*RC MAKALLA ATAKA USHIRIKISHWAJI WA VIJANA WA SCOUT KWENYE MATUKIO MBALIMBALI DSM*.




- Asema *umuhimu wao usionekane wakati wa Matukio ya majanga na Mikutano pekee.*


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* amemuelekeza *Afisa Elimu* wa Mkoa huo kuhakikisha kuanzia Sasa *Vijana wa Scout wanashirikishwa* Katika shughuli mbalimbali na sio kusubiri yatokee *Matukio ya Majanga, Mikutano, ugeni wa Viongozi au Misiba* ndipo umuhimu wao unaonekana.


*RC Makalla* ametoa maelekezo hayo wakati alipotembelewa ofisini kwake na *Kamishina wa Scout Dar es salaam* alieambatana na Watendaji wa *TAKUKURU* na kukabidhiwa *Kitabu Cha Mwongozo wa mafunzo kwa wawezeshaji kufundisha Vijana wa Scout kuhusu kuzuia na kupambana na Rushwa*.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.