Header Ads

DIWANI KANGA AAHIDI KUTATUA KERO ZA WANANCHI KATA YA KILAKALA.


DIWANI wa Kata ya Kilakala Manispaa ya Morogoro , Mhe. Marco Kanga, ameahidi kutatua kero za Wananchi wa Kata ya Kilakala ikiwamo ubovu wa barabara, uchakavu wa vyumba vya madarasa, pamoja, Maji , Soko  na Zahanati. 

Akizungumza na wananchi katika mkutano uliofanyika Oktoba 02/2021,  Mhe. Kanga, amesema, tangu aingie madarakani Decemba 2020 hadi June 2021 ameweza kutatua baadhi ya changamoto kwenye sekta mbalimbali katika kata hiyo.

“Changamoto kubwa tulizokuwa nazo ni katika sekta ya elimu kutokana na uchache wa vyumba vya madarasa, uchakavu wa sakafu na mabati, uhaba wa vifaa vya kufundishia, pamoja na uhaba wa vyumba vya waalimu,” Amesema Kanga.

Amesema, katika kukabiliana changamoto hizo, kwa kushirikiana na kamati ya maendeleo wamefanikiwa kufanya ukarabati wa miundombinu hiyo.

Ameendelea kusema kuwa pamoja na changamoto hizo,atahakikisha kwamba katika kuwainua kiuchumi wananchi wa Kata hiyo atasimamia vyema suala la mikopo ya Manispaa  na kuweza kuwasaidia wananchi hao  kuondokana na tatizo la ajira na kujikwamua kiuchumi.

Kuhusu suala la usalama, amesema wapo mbioni kujenga Kituo cha Polisi kwa ajili ya kufanya Kata hiyo kuwa Salama ikiwamo kulinda raia pamoja na mali zao.

“Rudini kwenye malezi waleeni watoto wajue Mungu, Ijumaa nenda nae mskitini, Jumapili nenda nae kanisani, Ijumaa nenda nae Msikiti hayo ndio malezi mazuri kwa Watoto wetu, tukijikita huko tutakuwa tunatengeneza vizazi vynye hofu ya Mungu na kujikuta Kata yetu inakuwa na Watu wema " Ameongeza Kanga.

“Mtoto apate muda wa kusoma Quaran apate kujua Mungu anasema nini uongo ni dhambi, kuua ni dhambi ndio makosa hayo hayo na kwenye nchi yanazungumzwa,” amesema na kuongeza.

Kwa upande wa Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Morogoro anayetokana na Kata ya Kilakala , Mhe. Mwanaidi Ngulungu, amesema atahakikisha kwamba anashirikiana bega kwa bega na wananchi katika kufikia malengo kwani kufanya hivyo kutasaidia kuiletea Kata hiyo maendeleo.

Mhe. Ngulungu, amesema kuwa kwa sasa jukumu kubwa ni kuona Kata ya Kilakala inapiga hatua katika nyanja zote .

"Nipo na Diwani wangu, wote tunaelekeza nguvu kuwatumikia wananchi wetu, Kata hii muda mrefu ilikuwa katika kiza sasa tunataka kuona mabadiliko, wametuchagua lazima tuwatumikia " Amesema Mhe. Ngulungu.

Katika Mkutano huo, ziliibuka hoja za changamoto ya maji, ambapo Diwani Kanga kwa kushirikiana na Mhe. Ngulungu wameahidi kuitatua kero hiyo mara moja.

Naye miongoni mwa Wananchi , Bwa. Emmanuel Masanja, amempongeza Diwani wa Kata ya Kilakala, pamoja na Diwani Ngulungu kwa kuitisha Mkutano huo ambao unalenga kutatua kero za pamoja.

"Nafikiri huu ndio Uongozi, wananchi tunachagamoto nyingi lakini kama tutashirikiana vyema na viongozi wetu tnaamini hizi changamoto zitatatuliwa" Amesema Masanja.






No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.