Header Ads

HOSPITALI WILAYA YA CHALINZE YAPOKEA VIFAA TIBA MILIONI 480 UNUNUZI VIFAA TIBA

Serikali imetimiza  ahadi zake zilizotolewa na Rais wa JMT Mh. Samiah Suluhu Hassan kwa kupeleka Vifaa tiba Hospitali ya Wilaya ya Chalinze vyenye thamani ya Shilingi Milioni 480 ikiwemo mashine ya Kupiga picha za Mionzi yaani X-Ray, Jokofu la kuhifadhia maiti, mashine za kupimia damu na vifaa mbalimbali.

Mh. mbunge wa Jimbo ameishukuru serikali kwa kutekeleza ahadi hii ndani ya muda wa wiki tatu toka kutolewa kwa ahadi.

Wananchi wa Kata hiyo wakiongozwa na wakina mama ambao walikuwa ipokea wameshangilia na huku wazee wakimuombea Mungu amlinde Rais wa Nchi yetu.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.