Header Ads

UWT MVOMERO WAMPONGEZA MBUNGE VITI MAALUM MKOA WA MOROGORO MH. NORAH MZERU


Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mvomero,  Lidya Joseph Mbiaji, akizungumza wakati wa Wiki ya UWT Wilaya ya Mvomero.

Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Mvomero  wamempongeza Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro , Mhe. Norah Mzeru,  kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi.

Pongezi hizo zimetolewa Oktoba 09/2021  kwenye maadhimisho ya Wiki ya UWT Wilaya ya Mvomero ambapo Mhe. Mzeru alikuwa mgeni rasmi.

Akizungumza kwa niaba ya wana UWT Wilaya ya Mvomero, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mvomero,  Lidya Joseph Mbiaji.amesema Mhe. Mzeru amekuwa akiwajibika sana na anafanya kazi kubwa kuhakikisha anawatumikia wananchi wake na kuwaletea maendeleo.

"Napenda kutumia fursa hii kumpongeza mbunge wetu wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe.  Norah Mzeru, kwa kweli mwanamke mwenzetu huyu anafanya kazi, Sisi kama wanawake wenzie tunajivunia uwepo wake na tutaendelea kumuunga mkono kwa kazi anazofanya," Amesema Mwenyekiti huyo.

Mwisho, amewaomba Wanawake wa CCM kumuunga mkono Mhe. Mzeru , kwani ni mwanamke ambaye anajituma sana na amekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Wilaya ya Mvomero pamoja na Chama .



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.