MBUNGE VITI MAALUM MKOA WA MOROGORO, MHE. NORAH MZERU, AGUSWA NA KIJANA MLEMAVU, AMPATIA KITI CHA KUTEMBELEA.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Mzeru, akiwa na Baba mzazi wa Naiphat Abdallah (kushoto).
MBUNGE wa Viti Maalum, Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Mzeru, amemsaidia Mtoto ajulikanaye kwa jina la Naiphat Abdallah, mwenye umri wa miaka 6 Mkazi wa Kata ya Mkindo Wilaya ya Mvomero, kwa kumpatia kiti cha kutembelea (Weelchair) pamoja na madaftari ili yamsaidie shuleni.
Ahadi hiyo ya kumasaidia kijana huyo , ameitimiza Oktoba 09/2021 katika Wiki ya UWT Wilaya ya Mvomero akiwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo.
“Nimeguswa na Binti huyu, nilipata taarifa kwamba kuna mtoto anatakiwa kusaidiwa , baada ya taarifa hiyo niliona ni vyema katika Siku hii ya leo nitimize ahadi yangu ya kumnunulia kiti kitakachomsaidia kuweza kufanya baadhi ya shughuli zake, na leo namkabidhi hiki kiti, haya yote tunayafanya sio kwamba sisi ni matajiri bali tupo hapa kwa ajili ya kumsaidia Mhe. Rais kazi , sisi kama viongozi tunayo majukumu ya kuhakikisha tunasaidia jamii" Amesema Mhe. Mzeru.
Naye Baba mzazi wa Naiphati Mohamed, amemshukuru Mbunge Mzeru kwa kumsaidia mwanae kwani sasa anauhakika kwamba Mtoto wake atatimiza ndoto zake za kusoma baada ya kupata usafiri wa kumpeleka shule.
Post a Comment