Header Ads

BENKI YA TCB YAZINDUA WIKI YA MTEJA YAAHIDI KUFANYA MAKUBWA KWA WATEJA WAKE

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Bw Sabasaba Moshingi, (wa pili kulia) akiongoza zoezi la kugongesha glasi kuashiria upendo na furaha kwa wateja wa benki hiyo wakati hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika leo Jumatano Oktoba 6, 2021 katika makao makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Rasilimali watu na Utawala Diana Myonga.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Bw Sabasaba akimkabidhi cheti Mteja wa Benki hiyo Goodluck Luhanjo, wakati hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika leo Jumatano Oktoba 6, 2021 katika makao makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam.

BENKI ya  Biashara Tanzania TCB  imesema hatua ya serikali kuweka mifumo imara  ya kifedha imezidi kuziboresha huduma za kifedha nchini ikiwemo kuongeza namba ya watu wanaotumia mifumo rasmi ya kifedha.

Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha wiki ya huduma Kwa wateja Mkurugenzi mkuu wa Benki hiyo Sabasaba Moshingi amesema   Nia Yao ni kutoa huduma  hasa kuwapa fursa wateja wadogo wadogo ambao ndiyo  azma ya Serikali na Benki hiyo ya Biashara ya Tanzania

Moshingi amesema kuwa nia yao nikusogeza huduma rafiki kwa wateja wake ili kuhakikisha kuwa  kila mtanzania wa hali ya chini anatumia benki hiyo kwaajili ya uendeshaji wa biashara zao katika Nyanja tofauti.

Kwa upande wao baadhi ya wateja na watumiaji wa mifumo ya kibenki wamesema kitendo Cha baadhi ya taasisi kuanzisha huduma za kuwajali wastaafu imezidi kuongeza weledi hivyo wameishukuru Benki ya TCB kwakuendelea kuwaamini nakuwawezesha kupata mikopo kwa wakati na kwamashart rafiki.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.