Header Ads

MBUNGE MZERU AWATAKA WANAWAKE KUREJESHA MIKOPO YA HALMASHAURI KWA WAKATI, AKIPA KIKUNDI CHA MBETE 200,000/= KUWAONGEZE MTAJI.

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Mzeru,(kulia) , akimkabidhi mmoja ya viongozi wa Kikundi cha Mbete kiasi cha Shilingi  200,000/= kwa ajili ya kuendeleza mtaji wao.
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Mzeru,(wapili kutoka kushoto), akiongozana na Mwenyekiti wa U.W.T CCM Wilaya ya Mvomero , Lidya Joseph Mbiaji. (kushoto) wakikagua bidha za Wajasiriamali.

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Mzeru, amewataka Wanawake  ambao wamenufaika na mikopo ya Halmashauri Mkoa wa Morogoro  kuhakikisha wanarejesha mikopo wanapewa kwa wakati ili fedha hizo ziweze kuvinufaisha vikundi vingi katika kujiletea maendeleo kama ilivyokusudiwa.

Kauli hiyo ameitoa leo  Oktoba 09/2021 katika  uwanja wa  Ofisi ya Kata ya Mkindo wakati wa kuadhimisha Siku ya  Wiki ya Umoja wa Wanawake Tanzania (U.W.T) Wilaya ya Mvomero ambapo Mhe. Mzeru alikuwa Mgeni rasmi katika Siku hiyo.   

Akizungumza na Wanawake mara baada ya kukagua bidhaa za Wajasiriamali hao na kuwaungisha , amesema fedha zinazotolewa na Halmashauri sio sadaka na wala sio ruzuku ya Serikali kwao ,bali zinatakiwa kurejesha ili ziweze kukopeshwa kwa wengine.

Mhe. Mzeru, licha ya kuwepo kwa mikopo hiyo, ameziomba Halmashauri kuongeza viwango vya mikopo kwa vikundi kuwa vikubwa ili hata pesa wanazokopa ziweze kuwa na tija badala ya kutoa mikopo midogo midogo ambayo haitakuwa na tija kubwa kwa wananchi.

"Nimeona niliseme hili leo, mikopo inatolewa na Halmashauri zetu lakini shida kubwa ni urejeshaji, niwaombe wakina mama wenzangu mliopata mikopo mrejeshe hiyo mikopo kwa wakati, pesa hizo sio za kuzichezea ngoma mmepewa ili muendeshe mitaji yenu na kuwanufaisha , lakini niombe sana Halamshauri zetu ,zitenge mikopo mikubwa yenye tija kwa vikundi,  ili wahusika waweze kuzalisha bidhaa bora badala ya kutoa fedha kidogo ambazo zinaiishia kwa wanakundi kugawana.  tukifanya hivi tutatoa fursa kwa wale wenye miradi yenye tija kuwaongezea thamani ya kupanua biashara zao, mikopo midogo midogo haina tija kwa vikundi vyetu," Amesema Mhe. Mzeru.

Aidha, amewaomba Wajasiriamali kufanya matangazo ya bidhaa zao wanazozizalisha badala ya kuziweka ndani ambapo ni vigumu wateja kuzifahamu na mwisho wa siku wanachelewa kuuza na kuchelewa kufanya marejesho.

Katika hatua nyengine, Mhe. Mzeru alikabidhi Kikundi cha Mbete kiasi cha Shilingi laki 350,000/=   kwa ajili ya kuwaongezea mtaji mara baada ya kikundi hicho kueleza changamoto zao wanazo kabiliana nazo.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.