Header Ads

MKURUGENZI MANISPAA YA MOROGORO ATAKA WAZEE WAPEWE KIPAUMBELE WANAPOFUATA HUDUMA.





MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Ally Hamu Machela, amewaagiza Wataalamu wafya pamoja na watumishi kutoa vipaumbele kwa Wazee wanapofuata huduma katikamOfisi zao.

Kauli hiyo, ameitoa leo Oktoba 1/2021 ikiwa  ni Siku ya Wazee Duniani ambapo kila mwaka Wazee wamekuwa wakienzi siku hii.

Akizungumza juu ya Siku ya Wazee Duniani, Machela, ametaka sehemu zote zinazotoa huduma  kutenga madirisha maalumu kwa ajili ya kuwahudumia wazee ili kuwaondolea usumbufu wa kupanga foleni.

"Wazee wetu ni hadhina, uzee haukwepeki, kila mtu hapa ni mzee mtarajiwa hivyo, kuna kila haja ya kuwatengea Wazee hawa madirisha ya kupata hudma ili Wazee hawa wasiweze kupanga foleni ndefu wanapokwenda kupata huduma kwenye ofisi hizo"Amesema Machela.

Amesema ,  wazee ni kundi linalohitaji kuhudumiwa haraka mahali popote wanapokwenda badala ya kuendelea kunyanyaswa kwa kupanga foleni kama watu wa makundi mengine.

Aidha, Machela, ameziomba   ofisi zote  za Serikali zilizopo Manispaa ya Morogoro  kuhakikisha zinatoa huduma kwanza kwa wazee ili wasiendelee kukaa sehemu hizo.

Katika hatua nyengine, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro , Dr Charles Mkombachepe, amesema  wazee wanatakiwa kupewa huduma ya haraka popote wanapokwenda.

“Wizara ya Afya ilishaagiza mzee ahudumiwe kwanza anapokwenda kupewa huduma kwenye hospitali zetu, nasisitiza hili kwamba wazee wetu wanatakiwa kuthaminiwa,” Amesema Dr. Mkombachepe .

Dr. Mkombachepe , amesema kwa sasa bado wanaendelea na zoezi la kugawa Vitambulisho vya msamaha wa Matibabu bure.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.