Header Ads

MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MOROGORO, MHE. NORAH MZERU AKABIDHI VIFAA ZAHANATI YA MKINDO.


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Mzeru, amekabidhi vifaa katika Zahanati ya Mkindo iliyopo Kata ya Mkindo Wilaya ya Mvomero.

Mhe. Mzeru, amesema  amekabidhi vifaa hivyo ni kupunguza changamoto zilizopo katika Zahanati hiyo ambayo imekuwa ikitumiwa na wananchi kupata huduma za afya.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Mkindo, leo  Oktoba 09/2021 ,Mhe. Mzeru ,amesema kuwa msaada wa vifaa hivyo ambavyo ni sabuni za kunawia mikono, sabuni za kusafishia sinki za vyoo, Gloves , mafagio huku akisema msaada huo ni moja ya  ahadi zake alizozitoa za kuwatumikia wananchi.

"Ndugu zangu leo nimekuja katika Zahanati hii ya Mkindo kukabidhi vifaa hivi muhimu ili kusaidia huduma ndogondogo katika  Zahanati hii ,  kwa hiyo vifaa hivi vitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto zilizopo hapa, leo wanawake wa CCM tunaadhimishi Wiki ya U.W.T hivyo katika kuadhimisha Siku hii niliona ni vyema nipitie hapa kuona changamoto za hapa lakini nikaona nisije mikono mitupu hapa najua zipo changamoto nyingi lakini tunaahidi kuzitekeleza kwa kuwa Serikali yetu ni sikivu chini ya Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassa, " Amesema Mhe. Mzeru 

Mhe. Mzeru, amekuwa na utaratibu wa kukutana na wananchi  katika Mkoa wa Morogoro kwenye mikutano ya hadhara kwenye kata na vijiji kwa lengo kuhakikisha Ilani ya CCM inatekelezwa kwa vitendo lakini pia kusikiliza changamoto walizonazo na kujadili namna ya kuzitatua.

Kuhusu suala la Shuka za Zahanati na Vituo vya  afya, amesema alishatoa shuka 100 zigawanywe katika vituo vya afya na Zahanati lakini cha kushangaza mpaka leo shuka hizo bado hazijasambazwa tangia mwezi wa 3 hadi leo mwezi Oktoba wakidai hawaja ziweka logo ya MSD.
" Kwa kweli nimesikitika sana kusikia mpaka leo shuka hazijafika hapa Zahanati, nikuombne Mhe. Diwani fuatilia hizi shuka zifike hapa ili wananchi waweze kunufaika nazo, sijafurahishwa, wananchi wamekuwa wakiilaumu Serikali haifanyi vitu kumbe kuna uzembe unafanyika huku chini, tusifanye kazi kwa mazoea tunapopata huduma ambazo zinatakiwa zifike kwa wananchi basi tutekeleze mara moja" Ameongeza Mhe. Mzeru.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.