Header Ads

TUMEPOKEA BILIONI 1.6 KWA AJILI YA KUTUMIKA SEKTA YA ELIMU NA AFYA - RIDHIWANI KIKWETE MBUNGE JIMBO LA CHALINZE.


MBUNGE wa Jimbo la Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete, amesema Halmashauri ya Chalinze imepokea Tshs  Bilioni 1.6 kati ya Mgawanyo wa fedha toka IMF Tshs. Trilioni 1.3.

Kikwete, amesema fedha hiyo ya Bilioni 1.6 zimeelekezwa kwenye sekta ya Elimu na X-ray kwa ajili ya huduma za Afya. 

Amesema kuwa pamoja na hilo ,Halmashauri ya Chalinze, imepokea  Tshs. Milioni 280 Mgao wa Tozo kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Msata, na Tshs. Milioni 80 kwa ajili ya Bweni la watoto wenye mahitaji maalim Shule ya Msingi Chalinze.

Amesema kuwa Mgawanyo wa fedha hizo  katika Sekta ya Elimu umeorodheshwa katika jedwali hapo chini .

 #FedhaZaMaendeleo #KaziIendelee #SSH #CovidRelief.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.