Header Ads

Kaimu Meya Ilala azindua semina ya Wasanii juu ya fursa za mikopo ya Halmashauri.






KAIMU Meya Wa Ilala, Omary Kumbilamoto, Leo amezindua rasmi semina ya wasanii kwenye Ukumbi wa  Anautoglo Jijini Dar Es Salaam.


Akizungumza na waandishi Wa Habari, amesema  lengo la  kuwa na semina hiyo elekezi kwa wasanii ni kuwaunganisha pamoja na kuweza kuwanyanyua kiuchumi na kupambana na umasikini.


Amesema kuwa semina hiyo ameifanya kufuatia agizo la  Mkuu Wa Mkoa wa  Dar es salaam, Mh Paul Makonda, la  kila Wilaya kuwajumuisha Wasanii kupatiwa fursa za mikopo. Amesema kazi za sanaa  zimekuwa nyingi na wasanii wanatoa kazi lakini maisha yao wanayoishi ni magumu.


" Nimefanikisha semina hii kikubwa ni kuangalia ni kwa namna  gani tunaweza kuwasaidia ndugu zetu wasanii hivyo tutahakikisha tunawashika mkono   na kuwa kwamua kiuchumi ili waishi vizuri " amesema Kumbilamoto.



 Naye Afisa Vijana Wa Manispaa ya Ilala, Spencia Masaga, amewataka wasanii hao wasiogope kukopa kwani Serikali ina  lengo zuri juu ya Vijana hao. Semina hiyo imehudhuliwa na Wasanii mbali mbali ikiwamo Bongo fleva, Vichekesho, Taarabu, Nyimbo za Injili, pamoja na ngoma za asili na vinyago.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.