Kaimu Meya Ilala aelezea jinsi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala watakavyoshirikiana na Forum CC katika mpango Wa Utunzaji Wa Mazingira pamoja na uboreshaji Wa mpango Mji.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Forum CC wamekutana na wataalamu, wadau wa mazingira kujadiliana namna Serikali itakavyoshirikiana na sekta binafsi katika utunzaji na uhifadhi mazingira pamoja na kuboresha mandhari ya mji.
Akizungumza katika mdahalo huo jijini Dar es Salaam Kaimu Mstahiki Meya wa manispaa hiyo, Omari Kumbilamoto amesema uboreshaji mandhari ya mji yanafanywa kwa kushirikiana na vyombo vya habari.
M
Amebainisha kuwa manispaa ya Ilala na Forum CC na kampuni za uzoaji taka pamoja na taasisi za fedha zinafanya juhudi za dhati kuhakikisha manispaa na mkoa zinakuwa katika hali ya usafi.
Amesisitiza kuwa katika mdahalo huo majadiliano yanalenga kuangalia serikali na sekta binafsi zitakavyoshirikiana kudhibiti mifuko ya plastiki.
Amefafanua kuwa matumizi ya mifuko hiyo ni makubwa kiasi cha kutishia mazingira,usalama wa mifugo, ndege, samaki pamoja na kuziba miundombinu ya maji ya mvua kusababisha mafuriko.
Pia amesema bado kuna maeneo mengi yanahitaji kuboreshwa ikiwemo kupanda bustani za maua, miti na majani ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Amempongeza Makamu wa Rais kwa kupiga marufuku matumizi ya mifuko hiyo.
Ameongeza kuwa katika kukabiliana na wingi wa takataka tayari manispaa imeongeza magari mawili makubwa.
Katika hatua nyingine amesema katika kukabiliana na ugonjwa wa Dengue manispaa hiyo imetenga sh milioni 52 huku akisisitiza hadi sasa wagonjwa 13 wa Kipindupindu wameripotiwa kati yao mmoja amefariki.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Forum CC, Rebecca Munda amesema wanafanya uhamasishaji wa mazingira kwa kushirikiana na serikali pamoja na wadau wengine.
Post a Comment