Header Ads

Dc Mjema aelezea hali ya Kipindu pindu Wilaya ya Ilala.






MKUU Wa Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema, amesema ugonjwa Wa kipindu pindu kwa ilala sio mkubwa sana.


Hayo ameyasema leo Ofisini kwake wakati Wa kusikiliza kero za Wananchi ikiwa ni utaratibu Wa Ofisi yake  na wataalamu wake uliojiwekea. Amesema tangia ugonjwa huo uingie Wilaya ya Ilala, wamepokea taarifa ya Wagonjwa 16 ambapo wagonjwa 6 wamelazwa katika Kempu ya Wagonjwa Wa Milipuko.

Amesema kuwa, ni mgonjwa mmoja tu aliyefariki dunia kutoka Kata ya Vingunguti.

Aidha amesema kipindu pindu hicho kimesababishwa na Maji machafu ya chooni yanayotiririshwa wakati Wa mvua.

 Amesema kuwa Maji hayo yanayotiririshwa yana sambaa kwenye maeneo ya makazi .


 " Wakati Wa ziara za kukagua maeneo yaliyoathirika na mafuriko , kuna maeneo kama Vingunguti na Mnyamani tumekuta vyakula sokoni vikisambazwa chini, hivyo wanapelekea kuhatarisha hali ya mlaji na kusababisha kipindu pindu kusambaa kwa kasi" Amesema DC Mjema.

 Hivyo, amewataka Wananchi kuhakikisha wanafanya Biashara zao katika hali ya usafi na Usalama na bidhaa zote zipangwe kwenye meza.


  Hata Hivyo, amepigia marufu Visima vifupi ambapo amesema visima Hivyo vingi  vipo Jirani na vyoo Hivyo Maji ya chooni na Yale yanayosambaa yanaingia na watu wengi hawachshi Maji na kupelekea Wagonjwa ya mlipuko kama kipindu pindu na kuharisha.


Amesema kuwa Waislamu wapo kwenye Mfungo Wa Ramadhani Hivyo wauzaji vyakula wahakikishe vyakula vinakuwa katika hali ya usafi na Usalama na vipashwe moto.

Amesema vimelea vya kipindu pindu havifii moja kwa moja kwani vinapoingia tumboni na hali ya jito vinaibuka upya na kushambulia mwili.

Pia amesema katika katazo LA mifuko ya plastiki , wamepigia marufuku Maji ya kandoro kwani wengi wao wanauza Maji bila kuchemsha.

Amewataka Bibi na Bwana Afya kutembelea maeneo ambayo machafu na maeneo ya vyakula ili kulinda Afya ya mlaji katika kujilinda na kipindu pind.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.