Header Ads

Kaimu Meya Ilala akutana na Waandishi wa habari TSJ kuzungumzia mikopo ya Manispaa






KAIMU Meya wa Manispaa ya ilala, Omary Kumbilamoto, amezungumza na wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa habari TSJ leo kwenye sherehe ya kuwakaribisha na kuwaaga wanafunzi.

Sherehe hiyo imefanyika Mei 3 , 2019  kwenye ukumbi uliopo South Beach Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari , Kumbilamoto , amewaasa wanafunzi hao walioagwa na wanaoingia wakope mikopo ya Manispaa kwani itawasaidia kujikwamua kiuchumi na kufikia malengo.


Amesema kuwa kiuhalisia katika watu wanaoishi masikini ni waandishi wa habari. .


Amesema waandishi wengi hawana mikataba katika ofisi zao hivyo maisha yao yanategemea na stori wanazoziandika jambo ambalo sio zuri sana kwa maisha ya sasa.

Aidha amewataka wanafunzi hao kuchangamkia fursa hiyo na kutengeneza mfumo mzuri wa maisha yao na familia zao.

 Amesema inafikia wakati mwandishi anaomba pesa kwa viongozi wakati tayari anauwezo wa kuandika  na kuitumia peni vizuri na maisha yakaenda vizuri" Amesema Kumbilamoto.


Pia amewataka maandishi hao Wa Habari kuandika na kuibua mambo yenye tija na ya Maendeleo yanayofanywa na Serikali Ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.