Dc Mjema akabidhi Viti 6 vya kubebea Wagonjwa na Walemavu Hospitali ya Amana.
MKUU Wa Wilaya ya Ilala , Mh Sophia Mjema, amekabidhi Viti 6 vya kubebea Wagonjwa na Walemavu katika Hospitali ya Amana Jijini Dar Es Salaam.
Hafla hiyo fupi ya makabidhiano ya Viti hivyo imefanyika Leo Hospitali ya Amana ambapo Kaimu Meya Wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto alihudhuria.
Akizungumza na Waandishi Wa Habari , Dc Mjema, ameupongeza Uongozi Wa Hospitali hiyo kwa kazi nzuri wanazozifanya katika kuwahudumia Wagonjwa.
Amewataka wauguzi na Madaktari waendelee kushikamana katika utoaji huduma kwani kufanya hivyo kunapelekea Wananchi kubwa na imani na Hospitali yao juu ya huduma bora wanazozipata. Pia amesema lazima Maadili ya kazi yazingatiwe na kuepuka vitu vidogo vidogo vinavyoweza kuwafanya wakachishwa kazi ambazo wamezifanya kwa muda mrefu.
Akizungumzia kuhusu Viti hivyo ambayo ni msaada Wa Wadau Wa Maendeleo kutoka Taasisi ya Bishara Njema Foundation, ameshukuru kwa kuwapongeza wadau hao katika jitihada za kuunga mkono Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli.
Amesema kwa hicho kidogo walichokipokea wao wamekiona ni kikubwa kwani kitasaidia sana kubebea Wagonjwa huku akiwaomba wazidishe moyo huo kwani bado Hospitali hiyo inakabiriwa na changamoto mbali mbali ikiwamo gari ya kubebea Wagonjwa ( Ambulance).
" Nipenda kuwashukuru sana Bishara Njema Foundation kwa msaada wao Mwenyezi Mungu awazidishie zaidi, lakini tunawaomba kama upo msaada mwengine tuleteeni kwani bado changamoto tunazo pia kama wapo wadau wengine tunawaomba wajitokeze kutusaidia Serikali hii inawahudumia watu wengi sana hivyo bado misaada ya wadau inahitajika.
Naye Kaimu Meya Wa Ilala, Mh Omary Kumbilamoto, ameupongeza Uongozi Wa Bishara Njema Foundation kwa niaba ya Manispaa ya ilala huku akisema bado wanahitaji wadau kwani zipo changamoto nyingi Wilaya ya Ilala ukiachilia Suala la Afya lakini Elimu, uhaba Wa Madawati na Vitendea kazi.
Amesema Bishara Njema Foundation wamefanya kitu kikubwa sana kwani walichokitoa kitasaidia sana katika Hospitali hiyo.
Kwa upande Wa Mwenyekiti Wa Bishara Njema Foundation, Bi Nunu , ameupongeza DC Mjema kwa kazi kubwa anayoifanya katika kubwa katibu sana na Wananchi wake.
Amesema ameshangazwa na kasi ya DC huyo kwani ni maana mama anayejua jinsi ya kushighulikia matatizo ya Wananchi wake.
" Tunampongeza ametupokea vizuri sana, huu ni mwanzo kwani pale tutakapojaliwa basi tutaungana nae tena kwa ajili ya kusukuma gurudumu la Maendeleo mbele, huu ni uzalendo Wa kumuunga mkono Rais wetu mpendwa Dkt John Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwatumikia Wananchi haswa masikini na Wanyonge" Amesema Bi Nunu Mwenyekiti.
Post a Comment