DC Mjema awataka waathirika Wa Mafuriko kuondoka maeneo hatarishi
MKUU Wa Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema, amewataka wale wote waliokumbwa na mafuriko na nyumba zao kujaa Maji wahame Mara moja.
Hayo ameyasema Leo Jangwani Jijini Dar es salaam Mara baada ya kukagua eneo hilo ambalo lilijaa maji na kuhatarisha maisha.
DC Mjema amesema kwa wale walionusurika na majanga wanatakiwa wasirudi maeneo hayo kwani bado mvua zipo kwa mujibu Wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania.
Akizungumza na waandishi Wa Habari, amesema lengo la Serikali kuwatembelea waathirika hao Wa mafuriko na kujaa Maji ni kuangalia jinsi ya kuwasaidia na kuwaokoa wale ambao wameshindwa kujiokoa.
Amesema mpaka sasa idadi ya watu walioathirika inafikia 635 na nyumba 522 zimeathirika ikiwamo Msikiti na Kanisa vimekumbwa na mafuriko.
" Tunamshukuru Mwenyezi Mungu hakuna hata mtu mmoja aliyepoteza maisha katika mafuriko haya, licha ya uharibifu Wa nyumba na Mali pia watu wameweza kujiokoa wenyewwe hiloni jambo la kumshukuru sana Mwenyezi Mungu " Amesema DC Mjema
Amewataka Wananchi wawe na subira katika kipindi hiki kifupi cha mpito kwani Serikali yao ni tulivu na ina wajali Wananchi wake.
Kuhusu miundombinu kama vile Makaraveti na bara bara amesema ukaratabi utafanyika baada ya hali ya hewa kuwa tulivu na kukatika kwa mvua.
Miongoni mwa maeneo aliyoyatembelea ni pamoja na Jangwani Kariakoo, Tabata Matumbi, Karakata Kata ya Kipawa na SIDO Kata ya Vingunguti.
Post a Comment