Header Ads

Tuwapuuze vibaraka, Tumpongeze Rais Dkt John Magufuli kwa kuupandisha uchumi wetu kwa kasi - Mwenyekiti Uvccm Msimbazi Jangwani




Uchumi wa Tanzania unakadiliwa kukuwa kwa zaidi ya 7% tangu Rais wa Tanzania Dr. John Joseph Pombe Magufuli kuingia Madarakani na kuiongoza Taifa hilo Katika Vita ya uchumi ambayo mpaka sasa Uchumi wa Taifa hilo umeendelea kuwa imara na ukiongoza katika nchi washiriki wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

Ni dhahiri shahili kuwa kuimarika kwa uchumi wa Taifa hilo unatokana na Umoja, Upendo, Amani na Mshikamano walionao watanzania. Watanzania wengi zaidi ya Mill 60,wamekua na KIU,Ali na hamu ya kuona Taifa lao linapiga hatua chanya Kimaendeleo. (Positive and sustainable Economic growth).

Aidha baadhi ya Wachumi nguli Duniani wanaonya kwa mataifa kadhaa kuwa  "Ni kosa kubwa kiuchumi kupandisha mishahara ya Watumishi HADHARANI" Athari zake ni kubwa kwa uchumi wa nchi ikiwa ni pamoja na kushitua misuli ya virusi vya uchumi (Economy virus muscles) kama, kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali  MFUMKO WA BEI, (inflation), Kushuka kwa thamani ya fedha, nk, nk,nk.

Mwanauchumi mmoja alisema "Taifa likiwa na Mwenendo mzuri wa UCHUMI ,Viongozi wajiepushe kutangaza misharara mipya HADHARANI. Msiruhusu Mishahara Kupanda". Katika falsafa ya UCHUMI, mfumuko wa bei (inflation) ukiwa mdogo huku pato la nchi nalo likiwa linaongezeka kistahimilivu (sustainably) ikiwa ni pamoja na kuruhusu AJIRA kuongezeka, pamoja na upatikanaji mzuri wa huduma muhimu za kijamii (access to social services)- kwa wakati huo ongezeko lolote la mishahara litakuwa hatarishi kwa Uchumi wa Taifa.

Watanzania ni mashahidi, Serikali ya Dr. John Pombe Magufuli imekuwa ikiboresha huduma za Kijamii nchi nzima, imekuwa ikitoa Ajira Katika sekta mbalimbali  ikwepo Elimu, Afya nk nk, Hii ni ishara tosha kiuchumi kuwa Kiongozi huyu wa Nchi ambaye amekuwa kivutio kikubwa kwa watanzania na nje ya nchi amedhamiria kwa dhati kulifanya Taifa la Tanzania kuwa Taifa lenye uchumi imara na mkubwa Duniani kupitia uanzishaji wa VIWANDA nchini.

Hivyo, katika agenda ya kujenga na Kuimarisha Uchumi wa Taifa na Wananchi, Kupandisha mishahara ni kuliingiza Taifa katika JANGA kubwa kiuchumi, Wananchi watateswa na BEI kubwa za bidhaa, Fedha yao itakosa thamani na Maisha hubadilika na jamii kukosa mahitaji muhimu ya kibinadamu. Wachumi wanashauri, cha msingi  katika uchumi unaokuwa vema SIO kutangaza ongezeko la mshahara HADHARANI BALI ni kuimarisha ufanisi  katika sekta za UCHUMI (Economic appetizers)  hasa katika maeneo nyeti kama Kudhibiti mfumuko wa bei (inflation)Kutoa Ongezeko LA ajira ( employment growth) na kukua kwa Pato la Taifa (growth in national income) and an ease to which people have access to social services such as education, security, health care, etc.

Hakika ,  Hatuna  budi kumpongeza Mh Rais wetu,kipenzi cha Watanzani . Dr. JOHN POMBE MAGUFULI kwa kufanikwa KURUKA KIHUNZI (barrier) HATARI KIUCHUMI, Tunaweza kumia nguvu nyingi na Muda mwingi wa kujenga na kuimarisha uchumi wa TAIFA letu, Lakini haichukui hata SEKUNDE moja kubomoa uchumi huo tuliotumia muda mwingi kuujenga na kuuimarisha. Nimpongeze sana Mh.Rais kwa  kutoweza kuharibu misingi imara iliyokwishajionyesha katika kila kiashiria tajwa hapo juu katika harakati ya kujenga na kukuza UCHUMI wa Taifa letu.

Sio Mimi nasema Bali Wale watu wanaotumiwa na MABEPARI/ MABEBERU wangesikia leo Mh.Rais ametangaza ongezeko la Mishahara mipya "Wangekaa vyumbani na kugonga class za Wine na kushangilia huku wakisema " WAMEJINYONGA WENYEWE.

Wakati wao wanaliombea MABAYA Taifa letu, kwa kujaribu kuwahadaa wananchi, sisi Watanzania tumeamua KUPIGA MAGOTI na Kumuombea Kiongozi wetu Dr. John Pombe Magufuli ambaye watanzania, Wake kwa waume, Watoto kwa vijana, Wazee na Watu wa kila aina zaidi ya Mill 60 tunamuombea kwa Mungu ili aendelee kuliongoza na kulivusha Taifa hili mpaka kuwa Taifa lenye ASALI na Maziwa.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Rais Wetu.

Asanteni Sana.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.