DC Mjema afungua Mashindano ya UMITASHUMTA Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
MKUU Wa Wilaya ya Ilala, Mh: Sophia Mjema, amefungua mashindano ya UMITASHUMTA Halimashauri ya Manispaa ya Ilala Leo kwenye Uwanja Wa Magereza Ukonga Jijini Dar Es Salaam.
Mashindano hayo ya UMITASHUMTA yamelenga kushirikisha Klasta nne (4), miongoni Mwa Klasta hizo ni pamoja na Klasta ya Chanika, Ukonga, Kimanga pamoja na Gerezani.
Akizungumza na Waandishi Wa Habari , DC Mjema, amewapongeza Waalimu na Wakufunzi kwa maandalizi mazuri ya ufunguzi huo Wa Mashindano.
Aidha, amesema kuanzishwa kwa mashindano hayo yanalenga katika kuunganisha undugu, ushirikiano Wa Shule za Msingi zote zilizopo katika Manispaa ya Ilala.
Pia amechukua nafasi ya kuipongeza timu ya Wilaya ya Ilala kwa kuchukua kombe kwa miaka 3 mfululizo katika Mashindano hayo.
Amewataka Wanafunzi wahamishe ajili zao katika Michezo na sio kujingiza na mambo yasiyo na tija kwao.
Amezitaka timu zote kuhakikisha zina cheza Michezo ya kiungwana na amani ili kuweza kupata timu nzuri itakayowakilisha ngazi za Mashindano ya Kiwilaya.
" Niwaombe Watoto zangu, mcheze vizuri mpendane tunataka tupate timu nzuri na tuzidi kuendelea kushikilia rekodi yetu kiwilaya, pia mchezaji yeyote atakaye jisikia vibaya amuone kiongozi wake apate matibabu ili kuzuia athari itakayoweza kujitokeza , Michezo inahitaji uwe na Afya bora" Amesema DC.
Pia Amesema atahakikisha mashindano ya UMITASHUMTA yana jitegemea na kuwa mazuri zaidi katika kuitangaza Wilaya ya Ilala.
Naye Kaimu Meya Wa Ilala, Mh Omary Kumbilamoto, amesema kuwa, Manispaa ya Ilala, ina Waalimu wazuri Wa Michezo hivyo ipo haja ya kuunda timu ya Mpira Wa Miguu ya Manispaa pasipo kutumia gharama kubwa.
Pia amempongeza Afisa Elimu Msingi Ilala kwa kazi nzuri anayoifanya ya kukuza Michezo katika Shule za Msingi na kuwapongeza Jeshi la magereza kwa kusaidia.
Miongoni Mwa Michezo itakayofanyika katika Mashindano hayo ni pamoja na Mpira Wa Pete, Netball, Handball, Mpira Wa Wavu, Riadha pamoja na fani za ndani.
Post a Comment