Header Ads

Dc Mjema ataka mfereji uliopo miradi Wa Reli ya Kisasa Maeneo ya Vingunguti na Kipawa utanuliwe.



MKUU Wa Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema, ameagiza Viongozi Wa TRC , YAP MARKEZ na uongozi wa  Manispaa ya Ilala, wakae pamoja waangalie utaratibu w kupanua mfereji huo.

Ameyasema hayo Leo akiwa Kata ya Vingunguti ikiwa  ni ziara yake ya pili kukagua Maeneo yaliyo athiriwa na mvua.

Akizungumza na waandishi Wa Habari amesema kuwa  mfereji huo  unahitaji kupanuliwa na Maji yake ya tiririke kuelekea mto  Msimbazi.

Pia amesema wao  Kama Serikali kazi yao  kubwa kukagua maeneo na kuwasaidia kutoa Pampu za kunyonya Maji.

Amesema mvua bado zipo hivyo Wananchi wachukue tahadhari na Viongozi waharakishe mfereji huo  unakamilika mapema  ili kuzuia athari kama ilivyo sasa.

Amesema  pia watahakikisha wanaifanyia matengenezo bara bara ya Vingunguti inayoelekea Machinjioni kwani imehariba sana.

 "  Huu ni msimu Wa mvua wataalamu chukueni hatua panueni mfereji kuokoa maisha ya Hawa Wananchi " Amesema DC Mjema.


Maeneo yaliyoatembelewa ni pamoja na Mtaa Wa Mtakuja na Miembeni Becco ambapo mtaa Wa mtakuja nyumba 5 na mtaa Wa miembeni nyumba 6 zimeathirika.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.