Header Ads

Kaimu Meya Ilala agawa Mikate kwa Wajane 170 Kata ya Vingunguti.



KAIMU Meya Ilala, Mh Omary Kumbilamoto, amegawa Mikate kwa Wajane 170 waishio Kata ya Vingunguti.

Zoezi hilo  la  ugawaji Wa Mikate limefanyika Shule ya Msingi Miembeni iliyopo Kata ya Vingunguti.

Akizungumza na Waandishi Wa habari , amesema lengo la  kugawa mikate hiyo ni muendelezo Wa kuwasaidia Wajane hao kwani amekuwa msaada mkubwa  sana Wa kuhakikisha Wajane hao wanapata huduma muhimu hususani suala la  Chakula.


Amesema hiyo sio Mara ya kwanza kwani amekuwa mlezi Wa kundi hilo  muhimu katika Kuona wanafikia mafanikio.

Amesema alichokitoa ni upendo kwa Wajane hao kutokana na kuguswa na maisha wanayoishi na Kuona njia peke ni kuwa  nao bega kwa bega .

" Hili ni kundi ambalo  linahitaji msaada kwani tegemezi wao  walishatangulia mbele za haki hivyo furaha yao ni kuwa  wanasaidia na ndicho ninachokifanya " Amesema Kumbilamoto.

Amesema hajaanza hapo kuwasaidia Wajane hao kwani hata muungano wao  umetokana na jitihada zake na hata katika Mikopo ya Manispaa amekuwa mstari Wa mbele Kuona Wajane hao wanapata mikopo na wanaendesha maisha yao.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.