Header Ads

Dc Mjema awatolea Uvivu wazazi wanao watelekeza Watoto.



MKUU Wa Wilaya ya Ilala , Mh: Sophia Mjema , amekemea vikali juu ya Wazazi wanaowatelekeza Watoto.

Hayo ameyasema Leo wakati Wa Kufungua Mkutano wa  mrejesho Wa Miradi kuzuia ukatili Watoto , Walemavu na Wanawake  Kata ya Kivule Wilaya ya Ilala.

Akizungumza na Waandishi Wa Habari, DC Mjema, amesema  katika Wilaya yake kamwe hatakubali vitendo hivyo kushamiri, hivyo atahakikisha wale wahusika wote Wa Vitendo hivyo wanachukuliwa hatua.

Amesema suala la  kutelekeza Watoto ni dhambi ambayo haiwezi kumuacha mtu  salama.

Amesema katika Wilaya yake anataka kuona  familia zina ishi kwa Amani na furaha.

Amewataka Wakina Mama wawafichue wale wa  Baba wenye  kuwatelekeza Watoto ili hatua za kisheria kufuatwa na kufikishwa Ustawi Wa Jamii au Mahakamani.

 " Wilaya yangu nataka Kuona hilo  suala linachukuliwa hatua, hata katika hali ya kawaida kitendo hicho cha kutelekeza Watoto kina kupa laana na hata  mambo yako hayafanikiwi " Amesema DC Mjema.

 Pia katika hatua nyingine amemtaka Kaimu OCD kuhakikisha ulinzi una imarika dhidi ya vitendo hivyo pamoja na vitendo vya unyanyasaji Wa kijinsia na ubakaji na wizi.

Amesema kuwa  atahakikisha wanakutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ili Kuona ni nani anaruhusiwa kutembea na kubeba  Visu na Mapanga bara barani.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.