Header Ads

DC Mjema afungua Mkutano wa mrejesho Mradi wa Ulinzi wa Watoto, Walemavu na Wakina Mama ngazi ya Kata ya Kivule.




MKUU wa Wilaya ya Ilala , Mh Sophia Mjema , Leo amefungua Mkutano wa marejesho ya miradi wa kupinga ukatili wa Watoto, Walemavu na Wakina Mama Kata ya Kivule.


 Mkutano huo umefanyika  kwenye Shule ya Sekondari Mbonea iliopo Kivule Mtaa wa Kerezange ambapo mradi  huo unatekelezwa.

 Akizungumza na waandishi wa Habari , DC Mjema, ameupongeza Uongozi wa Ajiso kwa kazi nzuri ya kujitolea kukamilisha miradi huo. Aidha amechukua nafasi ya kupongeza wafadhiri wa miradi huo, Probono kutoka Ujerumani kwa kufadhili mradi.

Licha ya mradi huo kutekelezwa Kata ya Kivule, amesema bado upo umuhimu wa elimu hiyo kusambaa katika Wilaya nzima ya Ilala. Amesema suala la Ukatili bado ni changamoto hivyo amewaomba Viongozi na Wanakamati kitumia fursa hiyo ili vitendo hivyo vitokomezwe.


Amesema Idadi kubwa katika takwimu Wilaya ya Ilala inaonesha Kata ya Kivule ina  ongoza kwa ukeketaji.

Amesema Watoto wakiendelea kukeketwa, wanapoteza uhai wa maisha yao wakati wa kujifungua.

" Kuna watu wana imani potofu wanafikiri wakiwakeketa watato zao wataolewa huo ni ujinga Tanzania tuna makabila 127 lakini hakuna mila hizo potofu kwani Mungu amemuumba Mwanamke na kipande  hicho sasa kikitolewa kina sababisha kuvuja kwa damu nyingi na kupelekea kifo" Amesema DC Mjema.

Amewataka Wale wote wenye  tabia  za kukeketa  Watoto zao waache Mara moja.

 Pia amewataka Wananchi kutoa taarifa kwa wale wenye  tabia  za vitendo viovu katika Jamii wafichuliwe na kutupwa Mahakamani.

Naye Mkurugenzi wa AJISO, Bibi Virginia Silayo, amesema mpakaka sasa wametoa elimu kwa wanafunzi juu ya ukatili na kuunda Klabu 9 zilizopo kata ya Kivule.

 Pia amesema kuwa wameanzisha mradi wa uzalishaji mali  kwa wahanga utakaosimamiwa na Kamati ya Kata(  mradi wa kilimo cha mboga mboga).

Amesema lengo ya Taasisi yao ni kuwasaidia Wanawake katika masuala ya kisheria .

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.