Waziri Kairuki awataka wafanyakazi wa shirika la maendeleo ya mafuta na petroli nchini(TPDC) pamoja na Wizara ya Nishati kuhakikisha kuwa magari wanayoagiza kwa ajili ya matumizi ya shughuli za serikali yawe yamefungwa mfumo wa kutumia gesi ili kuwa mfano wa kuigwa na wengine na kukuza sekta ya gesi asilia.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Uwekezaji Angela Kairuki amewataka wafanyakazi wa shirika la maendeleo ya mafuta na petroli nchini(TPDC) pamoja na Wizara ya Nishati kuhakikisha kuwa magari wanayoagiza kwa ajili ya matumizi ya shughuli za serikali yawe yamefungwa mfumo wa kutumia gesi ili kuwa mfano wa kuigwa na wengine na kukuza sekta ya gesi asilia.
Agizo hilo amelitoa leo Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 50 ya shirika la TPDC toka kuanzishwa kwake mwaka 1969 na baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa lengo la kuendeleza sekta hiyo.
Pia ameiagiza TPDC kuzipitia upya bei za gesi kwenye viwanda ili kuchochea uwekezaji sekta ya viwanda kwani kwa sasa asilimia 60 ya umeme katika gridi ya Taifa inatokana na umeme wa gesi asilia.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba amesema kwa mwaka huu wa Fedha unaoishia juni Shirika hilo linatarajia kupata faida ya shilingi billion 9 na kuacha kujiendesha kwa hasara na hatimaye kutoa gawio kwa Serikali.
Aidha ameongeza kuwa kwa sasa tayari mgari 200 yanatumia mfumo wa nishati ya gesi pamoja na Viwanda 44 ambavyo vinatumia nishati hiyo,huku jitihada mbalimbali bado zinaendelea kuhakikisha kuwa gesi inafika kwenye maeneo mengi hapa nchini
Hata hivyo ameongeza kuwa kunauhitaji mkubwa wa usambazwaji wa gesi ila kwa sasa wanaenda taratibu kutokana na upatikanaji mdogo wa fedha huku asilimia 60 ya Umeme unaotumika kwenye gredi ya taifa unatokana na gesWaziri asilia.
Post a Comment