HUMANITY FIRST TANZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA AHMADIYYA MUSLIM JAMAAT TANZANIA YAIKABIDHI SERIKALI MIFUKO 600 YA SARUJI KWA WAHANGA WA MAFURIKO HANANG
SHIRIKA la Humanity First Tanzania (Utu kwanza) kwa kushirikiana na Ahmadiyya Muslim Jamaat Tanzania, wameikabidhi Serikali mifuko 600 kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko ya matope yaliyotokea Hanang mkoani Manyara.
Akizungumza mara baada ya kupokea mifuko hiyo , Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Godfrey Kasekenya , ameishukuru Taasisis ya Ahmadiyya na Shirika la Humanity First Tanzania kwa msaada wao na kuwakimbilia waathirika wa Hanang.
Naye, Mratibu wa Shirika la Humanity First Tanzania Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala ya utoaji wa misaada mbalimbali katika Majanga kwa niaba ya Mwenyekiti wa Humanity First Tanzania, Shekh Abid Mahmood, amesema wametoa msaada huo kama kuwashika mkono waathirika wa mafuriko.
Shekh Mahmood, amesema shehena hiyo ya saruji 600 ni sawa na milioni 12.
Post a Comment