Header Ads

HAPA MNASTAILI PONGEZI KUWA NA MRADI HUU WA KIMKAKATI- MEYA JIJI LA MWANZA


HALMASHAURI ya Jiji la Mwanza  imetoa pongezi kwa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa utekelezaji mzuri wa mradi wa kisasa wa Stendi ya Mabasi Msamvu .

Pongezi hizo zimetolewa Desemba 06/2023 wakati wa ziara ya Jiji hilo la kufanya ziara ya kujifunza namna ya uendeshaji wa Stendi.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Meya wa Jiji la Mwanza  Mhe. Sima Costantine Sima, amesema kuwa kitendo cha Manispaa ya Morogoro kutekeleza miradi ya maendeleo ni moja ya hatua kubwa ya kuhakikisha ya kwamba wananchi wanapata huduma bora

“Tunawapongeza sana Manispaa ya Morogoro kwa kutekeleza miradi hii mikubwa ya maendeleo, soko kuu pamoja na kituo cha mabasi cha kisasa Msamvu ni hatua kubwa mno mmeifanya, tumeona mmefanikiwa jinsi ya kuwapanga wafanyabiashara wadogo wadogo, sisi tumekuja kujifunza kutoka kwenu na tunakwenda kutekeleza katika Halmashauri yetu.” Amesema Mhe. Sima.

"Hongereni Manispaa ya Morogoro kwa kuwa na miradi ya Kimkakati, tumejifunza mengi lakini kubwa, ni utaratibu wa uendeshaji wa Stendi namna ya ukusanyaji mapato, usimamizi wa Stendi , sisi tumeyachukua maelezo yenu tunakwenda kuyafanyia kazi na sisi Stendi yetu iwe moja ya kitega uchumi kikubwa katika Jiji letu" Ameongeza Mhe. Sima.

Kwa upande wa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro , Mhe. Paschal Kihanga, amepongeza Jiji la Mwanza  kwa hatua waliochukua ya kufanya ziara kwani Manispaa ya Morogoro imekuwa chuo cha mafunzo hususani katika miradi ya kimkakati.

Aidha kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Pilly Kitwana,  amesema kuwa uamuzi walioufanya wa kujenga kituo cha kisasa cha mabasi Msamvu ni chanzo kikubwa cha mapato kwenye Halmashauri.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.