WAZEE 150 KUPATIWA KADI ZA BIMA YA AFYA CHF KATA YA CHAMWINO- DIWANI MEYA
DIWANI wa Kata ya Chamwino, Mhe. Abdallah Meya, amesema ataanza na Wazee 150 sawa na Kaya 25 kwa ajili ya kuwezeshwa kupata kadi za Bima ya Afya ya Jamii (CHF) iliyoboreshwa ambapo amesema lengo ni kuona wazee wanaendelea kupata huduma za afya bure.
Kauli hiyo ya kugawa kadi kwa wazee , ameitoa Desemba 16/2023 katika maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyoathimishwa na Baraza la Wazee Kata ya Chamwino kwenye Makao ya watoto wenye utindio wa Ubongo na Viungo Amani Centre.
Mhe. Meya, amesema kupitia yeye pamoja na aliyekuwa mgeni rasmi Mwalimu ,Saida Selemani , wameona wagawe kadi hizo kusaidia wazee ikiwa ni njia ya kuteleza ilani ya chama cha Mapinduzi CCM.
“Kwa kuanzia tunatoa bima 150, dada yangu Saida atatoa bima 90 na mimi bima 60, zoezi hili litakuwa endelevu, lengo letu wazee wetu wapate huduma nzuri za afya na huduma hizi ambazo watakazopata wazee wetu zitakuwa za mwaka mzima , tuendelee kuwaunga mkono wazee kwa kuwa wazee ni hazina" Amesema Mhe. Meya.
Mwisho, Mhe. Meya , amewataka wananchi wa Kata ya Chamwino kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii.
Kwa upande wa Wazee ambao ni wanufaika wameshukuru jitihada za Diwani na Mgeni rasmi kwa kuwawezesha kujiunga na mifuko ya Bima ya Afya huku wakiwasii viongozi wengine kuiga mfano huo.
Katika maadhimisho hayo yalienda sambamba na uchomaji wa chanjo ya UVIKO-19 kwa Wazee, ambapo jumla ya wazee 27 walipata chanjo hiyo.
Post a Comment