MANISPAA YA MOROGORO YAJIPANGA KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO.
MANISPAA ya Morogoro imejipanga kuhakikisha inachukuwa tahadhari ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha.
Hayo yamezungumzwa na Afisa Afya Manispaa ya Morogoro , Ndimile Kilatu kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa katika kikao kazi cha Maafisa afya wa Kata kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa Desemba 8/2023.
Kilatu, amesema mvua zinazoendelea kunyesha ni chanzo kikubwa katika kusababisha magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na mengineyo.
"Tumekutana na Maafisa afya wa ngazi za Kata na timu yetu ya Manispaa , lengo la kikao chetu ni kujadili namna gani tutaweza kukabiliana na magonjwa haya ya mlipuko hivyo ni lazima tujiweke katika tahadhari linapotokea jambo tuwe katika namna nzuri ya kukabiliana nalo." Amesema Kilatu.
Kilatu, amewataka wananchi katika maeneo yao ya nyumbani kuendelea na desturi ya kuweka vitakasa mikono huku akiwataka Maafisa afya wa Kata kuendelea kutoa elimu ya usafi wa mazingira kwa jamii.
Post a Comment