MBUNGE WA WAFANYAKAZI ASIKILIZA KERO ZA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO
MBUNGE Viti maalumu anaye wakilisha Watumishi Tanzania Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora Mh. Dkt. Alice Kaijage ametembelea Manispaa ya Morogoro kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto za watumishi.
Akizungumza katika kikao hicho Desemba 15/2023 kabla ya kuwasikiliza watumishi hao Kaijage amewapongeza watumishi wa Manispaa ya Morogoro kwa kazi kubwa wanazofanya bila kujali changamoto nyingi wanazo kabiliana nazo katika utendaji kazi.
“Lengo la ziara yangu ni kusikiliza kero zenu watumishi na kuzisemea, najua zipo changamoto mnakumbana nazo lakini bado mmekuwa mkionesha uzalendo kwa kufanya kazi, nawapongeza sana , naamini changamoto hizi zitaenda kufanyiwa kazi na kupatiwa majawabu kwani Serikali ya Awamu ya 6 chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ni sikivu na inajali amslahi ya watumishi" Amesema Dkt. Kaijage.
Hata hivyo Kaijange mara baada ya kuwasikiliza watumishi hao amesema changamoto zote walizozitoa atazifanyia kazi ili kuhakikisha watumishi wanafanya kazi katika mazingira rafiki.
“Bajeti iliyopita kwa miaka mitatu eneo la utumishi halikuachwa na Serikali imeweza kubadilisha miundo na Kada ya watumishi 30,245 na imehuishwa na kusainiwa na kuanzakufanya kazi ilikuwa ni kilio cha miaka mingi”.
Kaijage amesema bajeti ya miaka mitatu watumishi zaidi ya laki nne wamepandishwa madaraja na kugharimu zaidi ya Shilingi Tilioni moja ikiwa upande wa malimbikizo ya mishahara Rais amegusa kwa miaka mitatu na ajira mpya zaidi ya laki moja na ajira elfu 21 Serikali za Mitaa.
“Nasema hayo kwasababu niko kazini Rais Samia ni msikivu amefanya kazi kubwa na anania njema na watumishi” Ameongeza Mhe. Kaijage.
Hata hivyo amesema Serikali ya awamu ya sita inagusa kila idara ikiwemo miradi ya Afya na Elimu,na watumishi ikiwa kwa muda wa miaka mitatu ameshusha fedha nyingi katika Halmashauri zote Tanzania hivyo ametoa rai kuendelea kumuunga mkono Rais kwa kufanya kazi kwa bidii.
Post a Comment