Header Ads

MANISPAA YA MOROGORO YAADHIMISHA WIKI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 62 YA UHURU KWA KUFANYA USAFI NA KUPANDA MITI

KATIKA  kuelekea wiki ya maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara, watumishi wa Manispaa ya Morogoro kwa kushirikiana na wananchi wamefanya usafi katika soko Kuu la Morogoro lililopo Kata ya Mji Mkuu pamoja na kupanda miti kando ya Mto Kikundi .

Akizungumza na watumishi na wananchi waliojitokeza kufanya usafi Desemba 07/2023 , Afisa Tarafa Manispaa ya Morogoro , Winfred Kipako,  amesema watumishi na wananchi wameungana kufanya usafi ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya  miaka 62 ya uhuru wa Tanzania bara ambapo maelekezo ya Kitaifa yametaka wananchi wajikite katika shughuli hizo.

Aidha,Kipako amepiga marufuku wananchi kuharibu mazingira kwa kutupa taka hivyo, huku akiitaka jamii kujenga tabia ya kutunza na kulinda mazingira yanayo wazunguka pamoja na kulinda vyanzo vya maji.


"Leo tumejumuika kufanya usafi wa pamoja, wito wangu kwa wananchi kila mtu awajibike kulinda na kutunza mazingira, lakini pia yale maeneo yetu ya wazi tujitahidi kupanda miti kama hatuna matumizi nayo ya kimiundombinu , Manispaa yetu inaelekea kuwa Jiji ni wajibu sasa zile taka tunazozalisha zihifadhiwe sehemu husika ipo miundombinu tumeiweka ya kuhifadhi taka itumike na sio kutupa taka hovyo jambo ambalo ni hatari kupata magonjwa ya milipuko" Amesema Kipako.

Naye Afisa Utamaduni Manispaa ya Morogoro, Safia Kingwahi, amewaomba wananchi pamoja na wadau ndani na nje ya  Manispaa kushiriki katika mdahalo wa mika 62 ya uhuru utakaofanyika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya Manispaa ya Morogoro tarehe 08/2023 kuanzia majira ya saa 2:30 asubuhi katika kujadili wapi Tanzania imetoka, ilipo na inapokwenda.

Tanganyika ilipata Uhuru tarehe 9,Disemba 1961 chini ya uongozi wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Rais wa kwanza  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.