DC CHONJO AZINDUA MRADI WA UGAWAJI WA VIWANJA 3504 ENEO LA STAR CITY KWA NJIA YA MTANDAO MANISPAA YA MOROGORO.
Meya Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga akitoa pongezi mara baada ya uzinduzi wa ugawaji wa Viwanja kukamilika. |
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina
Chonjo, amezindua na kukamilisha mradi mkubwa wa upangaji na upimaji wa Viwanja
3504 kwa njia ya Waandishi wa habari , kupitia njia ya mtandao Simu 'SMS'' katika Shamba la
Mwekezaji Star Infrastructure LTD
Manispaa ya Morogoro.
Zoezi hilo la uzinduzi limefanyika leo
Aprili 21, 2020 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza na Waandishi wa habari, amesema
upimaji na upangaji wa viwanja hivyo umetokana na Mwekezaji aitwaye Star
Infrastructure LTD ambae kwa hiari yao walikubali kumega sehemu ya Shamba lao
lenye ekari 1100 ili liweze kupimwa na Viwanja hivyo kukabidhiwa Wananchi waliovamia
sehemu ya eneo la Shamba hilo.
Amesema zoezi hilo lilifanyika baada ya
ramani usajiliwa kupitia Ofisi ya Mkurugenzi ambayo iliandaa utaratibu wa
kuanza ugawaji wa Viwanja hivyo mwezi Novemba 2019 lakini zoezi hilo lilisimama
kufuatia baadhi ya Wananchi kuwazua Wataalamu wa Idara ya Mipango Miji
walioenda kwenye eneo la mradi ili kufanya utambuzi wa Viwanja vilivyojengwa
ili kuepusha kuvigawa kwa watu wengine na kusababisha migogoro isiyo ya lazima.
Kufuata zoezi hilo ambalo lingetakiwa
kufanyika katika eneo la viwanja lakini kutokana na mlipuko wa Ugonjwa wa
CORONA , ndio maana ameamua kulifanya kwa njia ya mtandao wa ujumbe wa Simu ‘SMS”kupitia
vyombo vya habari.
Aidha, amesema kuwa Wananchi hao baada ya
kuwazuia Wataalamu walipeleka malalamiko yao kwa Mkuu wa Mkoa ambaye aliandika
barua Ofisi ya Mkurugenzi katka kupatiwa ufafanuzi wa namna zoezi
lilivyoendeshwa ambapo Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ilijibu barua hiyo.
"Tupo hapa kwa ajili ya uzinduzi wa
mpango wa ugawaji wa Viwanja kwa njia ya simu leo, lakini niseme tu mpango huu
tulishauanza muda mrefu wapo baadhi ya Wananchi walitaka kuharibu mpango huu ,
lakini Ofisi ya Mkurugenzi ilipokea maelekezo kutoka Ofisi ya Mkuu waa Mkoa ya
kuitaka kuendelea na zoezi la ugawaji wa Viwanja hivyo chini ya usimamizi wa
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya mwezi Machi 2020, baada ya kujiridhisha kuwa malalamiko
yaliyopelekwa hayakuwa sahihi, nashukuru na kuipongeza Ofisi ya Mkurugenzi
pamoja na Baraza la Madiwani kwani Ofisi ya Mkurugenzi iliwasilisha taarifa ya
utaratibu uambao ulifanyika wa ugawaji wa Viwanja hivyo katika kikao cha Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya (KUU) cha mwezi Machi 2020" Amesema DC
Chonjo.
Katika hatua nyengine, DC Chonjo, amesema
kuwa kwa mujibu wa makubalian ya ugawaji wa Viwanja katika mradi huo
umezingatia makundi makubwa matatu ambayo
miongoni mwao ni Wananchi 1765 waliovamia shamba hilo la mwekezaji, kundi la pili ni la Wananchi 547 ambao Viwanja vyao vilikuwa na changamoto mbalimbali kama vile
miliki pandikizi, viwanja vilivyotolewa katika maeneo yenye makongor , viwanja
hewa pamoja na Wananchi waliojenga kwenye hifadhi mbalimbali (Mito, barabara na milima), kundi la tatu ni
Wakulima 97 waliojitoa katika kesi kati yao na Manispaa waliokuwa na mashamba
katika maeneo ya Lukobe na Kihonda au wale ambao walifungua mashauri yao kwa
kuishtaki Manispaa na baadae wakakubali kuondoa mashauri hayo kwa masharti ya
kupewa Viwanja mbadala.
Hata hivyo DC Chonjo, amesema kuanzia tarehe 21 , Aprili mwaka 2020 uzinduzi
rasmi wa ugawaji wa Viwanja kwa njia ya Vyombo vya habari umeanza rasmi, ambapo
wananchi watatakiwa kufika kwa makundi ya kati ya watu 50-100 kwa siku za
Jumatano na Ijumaa ya kila wiki hivyo wananchi 50 wa mwanzo watafika Ofisi za
Ardhi tarehe 22/4/2020.
Amesema Majina ya watakopata Viwanja
yatabandikwa kwenye mbao za matangazo katika Ofisi za Kata na Mitaa, Ofisi za
Ardhi, Ofisi ya Mkurugenzi ambapo wataona tarehe ya kufika kwa ajili ya
kuhudumiwa huku akitoa angalizo kwa wale ambao hawataona majina yao wasubirie
utaratibu mzuri ambao unaandaliwa.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amewaomba
Wananchi kutoa ushirikiano kwa Wataalamu wa ardhi kwani shughuli hiyo haikuwa
raihisi hadi kufikia kugawa Viwanja.
"Tumekuwa tukipambana sana kuhakikisha
zoezi hili linakamilika, sasa kikubwa ni wananchi waendelee kuta ushirikiano ili
zoezi hilo likamilike, kama hujatumiwa Ujumbe wa SMS usiende zoezi hli
litafanyika kwa hatua pale uanapopata ujumbe kwa simu yako tafadhali fika e
neo
husika uliloambiwa uende kwa kufanya hivi sitegemei kutokea kwa vurugu ya aina
yoyote na tutamaliza salama maana Manispaa yetu imefanya jambo hilo kwa faida
yenu" Amesema Mhe. Kihanga.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Manispaa ya
Morogoro, Sheilla Lukuba, amempongeza
Mkuu wa Wilaya, Baraza la Madiwani likiongozwa na Mhe. Pascal Kihanga pamoja na
Ofisi ya Mipango Miji kwa kukamilisha zoezi la ugawaji na upimaji wa Viwanja.
“Tumekamilisha hatua nzuri na yakupongezwa,
kazi hii haikuwa rahisi, zipo changamoto mbalimbali zilijitokeza lakini chini
ya Uongozi wa Mkoa, Wilaya , Baraza la Madiwani Manispaa ya Morogoro walifanya kazi nzuri
iliyotufikisha hii leo hadi tunazindua ugawaji huu wa Viwanja, ombi langu kwa
wananchi washirikiane vyema na timu ya Wataalamu wa ardhi ili wasije
kuturudisha tulipotoka, nawaomba Wananchi wawe watulivu ili zoezi hili
limalizike kwa usalama “ Amesema Sheilla.
Aidha amesema zipo hatua kadhaa ambazo
zilichukuliwa kuhakikisha kwamba zoezi hilo linakamilika kwa usalama na
utulivu.
Miongoni mwa hatua ambazo Ofisi ya
Mkurugenzi ilizichukua ni pamoja na kufanya uhakiki wa ndani kuona Viwanja
vilivyojengwa ili kutovigawa kwa watu wengine ili wale waliojenga kabla ya
upimaji wabaki katika viwanja hivyo, kuandika barua kwa Wateja wote waliokuwa
wanastahili kupata Viwanja kwa kutaja namba ya kiwanja na kitalu na namba hizo
kuingizwa katika mfumo wenye majina yao, kuandika majina yaliyopitishwa
/kubaliwa na tume / vikao na kuyawasilisha kwa Mkuu wa Wilaya na nakala kwa
katibu Tawala Mkoa, Ofisi za Kata pamoja na za Mitaa, kuwapeleka Site kuonesha
viwanja kila siku ya Jumatano na Ijumaa ya kila wiki pamoja na kukamilisha wale
wote watao lipia gharama za hati baada ya kuona majina yao na viwanja.
Post a Comment